Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Serikali nchini Australia yaanza kuwahamisha wananchi wake kwenye maeneo ya bondeni kuhofia mafuriko

Maelfu ya wananchi wa Australia wameanza kuhama kwenye maeneo yao kusini mashariki mwa nchi hiyo kufuatia miji mingi kuhofiwa kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. 

Nyumba zikiwa zimefunikwa na maji nchini Australia kutokana na mafuriko ambayo yanahofiwa tena kuikumba nchi hiyo
Nyumba zikiwa zimefunikwa na maji nchini Australia kutokana na mafuriko ambayo yanahofiwa tena kuikumba nchi hiyo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa nchi hiyo Julia Gilard amesema kuwa vikosi vya jeshi vimeanza kusambazwa kwenye miji ya New South Wales, Queensland na Victoria ambako mafuriko hayo yanatarajiwa kuwa na athari.

Tayari serikali imetangaza hali ya hatari kwenye miji hiyo na kuwataka wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya mabondeni na maeneo ambayo mwaka jana yalikumbwa na mafuriko kuhama mara moja.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini humo imesema kuwa tishio hilo linatokana na kuendelea kuja kwa mto Murrumbidgee ambao muda wowote unatarajiwa kufurika na kupasuka kingo zake hali ambayo itahatarisha usalama wa wananchi kwenye miji hiyo.

Tayari watu zaidi ya elfu nane wamekiwishaanza kuhamishwa kwenye mji wa Waga wagga ambao tayari athari za mvua hizo imenza kuonekana ambapo wananchi wake wanahamishiwa kwenye maenei salama.

Umeme umeanza kuzimwa kwenye baadhi ya maeneo ambayo huenda yakakumbwa na mafuriko ili kuzuia athari ambazo zinaweza kutokan na umeme.

Nchi ya Australia mwaka jana ilikumbwa na mafuriko makubwa mabayo yalisababisha miundo mbinu mingi kuharibiwa ikiwemo mji wa Queensland ambao uliathirika kwa kiasi kikubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.