Pata taarifa kuu
Cambodia

Mahakama kutoa hukumu dhidi ya mwanamke anayetuhumiwa kwa mauaji ya halaiki nchini Cambodia

Mahakama ya Umoja wa Mataifa mjini Cambodia juma lijalo itatoa hukumu kuhusu kuachiwa huru kwa mke wa aliyekuwa kiongozi wa kundi la Khmer Rouge, Ieng Thirith baada ya kuonekana kuwa hastahili kuendelea na mashitaka yanayomkabili kutokana na matatizo ya afya ya akili.

Wananchi wa Cambodia wakiwa katika moja ya maandamano
Wananchi wa Cambodia wakiwa katika moja ya maandamano
Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita majaji wa mahakama hiyo waliagiza kuachiwa huru kwa mwanamke huyo pekee ambaye amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za makosa ya mauaji ya halaiki.

Majaji wa Mahakama hiyo walitoa agizo hilo baada ya wataalamu wa afya kusema kuwa mwanamke huyo anakabiliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu.

Hata hivyo waendesha mashtaka walipinga suala hilo na kulipeleka katika mahakama kuu ya rufaa ambayo huwa na kikomo cha siku 15 kufanya maamuzi ya mwisho.

Hata hivyo kikomo hicho kimesogezwa mbele kwa juma moja hadi Disemba 13 kufuatia majaji kusema kuwa suala hilo ni jipya kufanyika, hivyo linahitaji muda kulishughulikia.

Pamoja na rufaa hiyo kupinga kuachiwa kwa mwanamke huyo,inaonekana kuwa si rahisi mwanamke huyo kuendelea kujibu tuhuma zinazomkabili dhidi ya mauaji ya halaiki, uhalifu wa kibinadamu na uhalifu wa kivita kutokana na madaktari kusema kuwa si rahisi hali yake kuimarika.

Ieng Thirith ni mwanamke pekee katika kudi la Khmer Rouge ambalo linadaiwa kusababisha mauaji ya watu wapatao milioni mbili katika kipindi cha mwaka 1975 hadi 1979.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.