Pata taarifa kuu
THAILAND

Waziri Mkuu wa Thailand atangaza mafuriko ya Bangkok kudumu kwa majuma manne

Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra ameonya mafuriko ambayo yameukumba Mji Mkuu Bangkok yanaweza kudumu kwa majuma manne zaidi wakati huu ambapo juhudi za kudhibiti maji hayo zikizidi kushika kasi huku viwanja wiwili vya ndege vikiwa vimeshafungwa.

© Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Yingluck amewaambia wanahabari kuwa mafuriko ambayo yapo katika Mji Mkuu wa Bangkok yatadhibitiwa ili yasiweze kuleta madhara makubwa wakati huu ambapo nchi yake inashuhudia mafuriko mabaya zaidi katika miongo kadhaa sasa.

Kiongozi huyo amesema anaimani kwa asilimia hamsini eneo la Ukanda wa Bangkok hauwezi kufunikwa kabisa na mafuriko ambayo yamechangiwa pakubwa na mvua ambazo zimenyesha tangu mwezi Julai mwaka huu.

Tamko hili linakuja huku kikiwa na hofu huenda Jiji la Bangkok likakumbwa na mafuriko zaidi ambayo yamechangiwa na kujaa kwa Mto Chao Phraya lakini Waziri Mkuu amesema hakutakuwa na madhara ya aina yoyote.

Waziri Mkuu Yingluck ameongeza kuwa kwa namna ambavyo wanashughulikia tatizo hilo wanaweza kulimaliza katika kipindi cha majuma mawili au moja na hali ikarejea kama ilivyokuwa awali.

Kwa sasa wananchi wanakabiliwa na uhaba wa maji salama ya kunywa huku maduka mengi yakiwa yamefungwa kutokana na wafanyabiashara kushindwa kufanya shughuli zao kwa sasa kulingana na mazingira yaliyopo.

Shule na ofisi za serikali zimefungwa kwa sasa na serikali imezitaka kampuni za umma na zile za binafsi kuwaruhusu wafanyakazi wake kuwapa mapumziko lakini Benki Kuu imesema masoko ya hisa yataendelea na shughuli zake.

Zaidi ya watu mia tatu na sabini wamepoteza maisha katika kipindi cha miezi mitatu tangu kuanza kwa mgogoro huu wa mafuriko huku wengine zaidi ya elfu nne wakilazimika kuyahama makazi yao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.