Pata taarifa kuu
THAILAND

Mafuriko Nchini Thailand yasababisha Viwanja viwili vya ndege kufungwa

Mafuriko ambayo yameikumba nchi ya Thailand yameendelea kuleta madhara makubwa na kuchangia Uwanja wa Ndege wa pili kulazimika kufungwa na kuahirisha safari zote kutokana na kuanza kuzingirwa na maji.

REUTERS/Bazuki Muhammad
Matangazo ya kibiashara

Uwanja wa Ndege wa Don Muang ambao unatumika kutua na kuruka ndege za ndai umelazimika kufungwa kutokana na maji ya mafuriko hayo ambayo yametokea Kaskazini mwa nchi hiyo kuonkena kutishia usalama wa safari.

Uwanja huo unatajwa kuweza kuhudumia jumla ya ndege mia moja kila siku zile ambazo zinatua na kuondoka na kufungwa kwake kuna maana huduma hiyo ya usafiri haitopatikana kwa wateja.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa uliopo katika Mji Mkuu Bangkok wenyewe bado unaendelea kufanya shughuli zake kutokana na kutokumbwa na madhara ya maji hayo ya mafuriko yanayoendelea kusambaa nchini Thailand.

Maji ambayo yamejaa kwenye maeneo mbalimbali nchini Thailand kwa sasa yameanza kuongozwa katika eneo la Kusini la nchi hiyo kwa jili ya kuingizwa Baharini huku vifuko vya mchanga vikiweka maeneo mbalimbali kudhibiti maji hayo.

Nchi ya Thailand imeshuhudia mvua za masika ambazo zilinyesha kuanzia mwezi Julai na kuchangia kutokea kwa mafuriko katika sehemu ya nchi hiyo na kuchangia watu mia tatu na sitini kupoteza maisha hadi sasa.

Mapema leo Baraza la Mawaziri nchini Thailand limeidhinisha dola bilioni kumi nukta tano kwa ajili ya kuijenga upya nchi hiyo huku walengwa wakubwa wa fedha hizo wakiwa ni wafanyabiashara wadogo ambao wameathirika na mafuriko hayo.

Waziri wa Fedha Thirachai Phuvanatnaranubala amesema fedha hizo zitatolewa kuwasaidia wafanyabiashara hao ambao inaaminika kama wataweza kurejea na kufanya biashara zao basi watasaidia kukuza uchumi wa taifa hilo.

Naye Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra ambaye anakutana na mtihani wa kwanza tangu aingie madarakani amesema watahakikisha wananchi wanahifadhiwa katika maeneo salama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.