Pata taarifa kuu

Dani Alves ahukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu jela kwa kosa la ubakaji

Mbrazil Dani Alves, nyota wa zamani wa Barca na PSG, amehukumiwa Alhamisi na mahakama ya Barcelona kifungo cha miaka minne na nusu jela kwa kosa la kumbaka msichana mdogo katika klabu ya usiku jijini humo Desemba 2022.

Dani Alves wakati wa mechi kati ya klabu yake ya Pumas na Atlas kwenye uwanja wa Jalisco huko Guadalajara, Mexico, Septemba 3, 2022.
Dani Alves wakati wa mechi kati ya klabu yake ya Pumas na Atlas kwenye uwanja wa Jalisco huko Guadalajara, Mexico, Septemba 3, 2022. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Kuna ushahidi ambao, zaidi ya ushuhuda wa mlalamishi, unawezesha ubakaji kuchukuliwa kuwa umethibitishwa," mahakama imesema katika taarifa.

"Mshtakiwa ghafla alimshika mlalamikaji, na kumwangusha chini na kupenya ukeni, na kumzuia asitikisike, huku mlalamikaji akisema hapana na alitaka kuondoka," amesema.

Alves, ambaye amekuwa kizuizini kabla ya kesi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja na atakata rufaa dhidi ya uamuzi huu, kwa mujibu wa wakili wake, pia ameagizwa kulipa euro 150,000 kwa msichana huyo na kukaa mbali naye kwa miaka tisa na nusu, pamoja na miaka mitano ya kuachiliwa kwa kufuatiliwa mara baada ya kifungo chake kutekelezwa.

Katika uamuzi wake, mahakama iliangazia vidonda kwenye magoti ya mwathiriwa, na kuvielezea kama "matokeo ya vurugu iliyosababishwa na Bw. Alvès".

Aidha Mahakama imesema kuwa ushahidi wa mwathiriwa umekuwa "sawa" wakati wote wa utaratibu na kwamba hakuwahi kutaka kupata "maslahi ya kiuchumi" kutokana na jambo hili.

- Adhabu ndogo kuliko ilivyoombwa -

Hukumu ya Alves, 40, mwishoni mwa kesi hii iliyotangazwa sana, ambayo ilifanyika mapema Februari, ilizua hisia hata kutoka kwa serikali ya mrengo wa kushoto ya Uhispania, ambayo ilipitisha sheria yenye utata juu ya idhini mnamo 2022 ya ngono ya wazi.

"Imekwisha!" ametangaza nambari tatu katika serikali, Waziri wa Kikomunisti wa Kazi Yolanda Diaz, akimaanisha kauli mbiu ya timu ya mpira wa miguu ya wanawake baada ya busu la kulazimishwa mwaka jana la mkuu wa zamani wa Shirikisho Luis Rubiales kwa mchezaji Jenni Hermoso.

"Hakuna udhalimu tena, hakuna unyanyasaji wa kijinsia tena! Natumai hii itakuwa kama hatua ya kupigiwa mfano," ameongeza katika korido za Bunge.

Adhabu iliyotolewa kwa Alves, hata hivyo, ni ndogo sana kuliko miaka tisa iliyoombwa na upande wa mashtaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.