Pata taarifa kuu

Mioto mikali ya misitu nchini Chile: Hali ya dharura yatangazwa

Juhudi za kutoa msaada zinaendelea Jumamosi hii, Februari 3, nchini Chile ambapo hali ya kipekee imetangazwa siku moja kabla ili kupambana na moto mkali wa misitu unaoenea katika maeneo ya kitalii ya nchi hiyo ya Amerika Kusini. Ripoti ya muda inabaini karibu vifo kumi.

Wakaazi huko Vina del Mar (Chile) wahamishwa, Februari 2, 2024.
Wakaazi huko Vina del Mar (Chile) wahamishwa, Februari 2, 2024. AFP - JAVIER TORRES
Matangazo ya kibiashara

 

Moto unaoikumba Chile umetumbukiza eneo la mapumziko maarufu la bahari la Vina del Mar (katikati), kando ya pwani ya Pasifiki, katika eneo la Valparaiso kwenye wingu la moshi; unatishia mamia ya nyumba, na kusababisha uhamishaji wa lazima. Wazima moto wamekuwa wakipambana bila kuchoka tangu Februari 2 dhidi ya karibu nyumba kumi katika mikoa ya Valparaíso na O'Higgins katikati, lakini pia Maule, Biobío, La Araucanía na Los Lagos, kusini. Katika miji ya Estrella na Navidad, kilomita 200 kusini-magharibi mwa mji mkuu, moto usiodhibitiwa uliteketeza karibu nyumba thelathini, na kuwalazimisha wakaazi kukimbilia eneo hili karibu na eneo la mapumziko la bahari la Pichilemu, maarufu kwa kuteleza.

Halijoto ni karibu 40° katikati mwa nchi

Tangu Jumatano Januari 31, hali ya joto imekuwa karibu na digrii 40 katikati mwa Chile na mji mkuu Santiago. "Tuna taarifa za awali zinazoonyesha watu kadhaa wamekufa, karibu kumi," ametangaza Sofía Gonzáles Cortés, mwakilishi wa serikali katika jimbo la Valparaiso. Rais wa Chile Gabriel Boric alitangaza hali ya hatari ili "kuwa na njia zote muhimu" katika kukabiliana na kuendelea kwa moto huo. "Vikosi vyote vimetumwa katika mapambano dhidi ya moto wa misitu," aamesema Mkuu wa Nchi katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani ukiitwa Twitter). Mkutano wa huduma za dharura unaitishwa Jumamosi asubuhi ili kufanya tathmini ya awali ya hali hiyo.

Zaidi ya heka 7,000 zateketezwa na moto

Katika eneo la Valparaiso pekee, moto huo umeteketeza zaidi ya heka 7,000, kulingana na CONAF, ofisi ya kitaifa ya misitu ya Chile, ikionyesha "mabadiliko makubwa" ya moto huo. Picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, zilizopigwa na madereva wa magari waliokwama, zinaonyesha milima ikiwa imeteketea kwa moto mwishoni mwa barabara 68, barabara inayotumiwa na maelfu ya watalii kwenda kwenye fuo za Pasifiki. Mamlaka pia ilikatiza safari katika eneo hilo siku ya Ijumaa kwa sababu ya "kupungua kwa mwonekano kwa sababu ya moshi".

Joto hili linalotokana na mfumo wa hali ya hewa ya El Niño kwa sasa linaathiri koni ya kusini ya Amerika ya Kusini, katikati ya kiangazi, na kusababisha moto wa misitu kuwa mbaya zaidi kutokana na ongezeko la joto duniani. Baada ya Chile na Colombia, wimbi la joto linatishia Argentina, Paraguay na Brazil katika siku zijazo.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.