Pata taarifa kuu

Brazili: Kuanguka kwa mgodi wa chumvi kunaongeza hatari ya "janga la mijini"

"Kuporomoka" kwa mgodi wa chumvi huko Maceio, kaskazini-mashariki mwa Brazili, kunaongeza hatari ya "janga la miji" kulingana na mamlaka na watu wanaoishi karibu na eneo wamehamishwa.

Mnamo Machi 20, 2022, huko Petropolis (Jimbo la Rio de Janeiro), mvua kubwa iliyonyesha ilisababisha maporomoko ya matope katika kitongoji cha Vila Felipe. (Picha ya kielelezo)
Mnamo Machi 20, 2022, huko Petropolis (Jimbo la Rio de Janeiro), mvua kubwa iliyonyesha ilisababisha maporomoko ya matope katika kitongoji cha Vila Felipe. (Picha ya kielelezo) © Sarah Cozzolino
Matangazo ya kibiashara

Meya wa mji mkuu wa jimbo la Alagoas Joao Henrique Caldas aliripoti siku ya Ijumaa kwenye kituo cha CNN hatari "inayokaribia" na "janga kubwa zaidi la mijini linaloendelea ulimwenguni".

Kulingana na maafisa wa Ulinzi wa raia, hatua za mwanzo zimewezesha kuwalinda wakaazi, lakini hawataepuka maafa ya kiikolojia.

Maelfu ya familia zilihamishwa tena Jumatano, mchakato wa kuhama ambao ulianza mnamo mwaka 2019 mara tu hatari katika eneo hili zilipojitokeza.

Vitongoji vinavyotishiwa ambapo watu 55,000 wamekuwa wakiishi katika zaidi ya majengo 14,000 ya makazi ni tupu.

Mgodi mkubwa uko chini ya usawa wa bahari na kuanguka kwake kunahatarisha kuwa na athari kubwa kwa mazingira.

Ili kuelezea jambo hilo, kikosi cha ulinzi wa raia kilichukua picha ya sinki ambalo mfereji wa maji huondolewa ghafla: kiasi kikubwa cha chumvi kitatiririka ghafla ndani ya maji na kuvuruga mfumo wa ikolojia wa baharini.

Shughuli mbalimbali karibu na mgodi huo zimepungua kabisa. Kiwango chake kimeshuka kwa sentimeta 11.4 katika muda wa saa 24 zilizopita, tena kulingana na kikosi cha ulinzi wa raia.

Na tangu Novemba 21, eneo hilo limezama kwa mita 1.43, chanzo hiki kimebaini.

Mgodi wa chumvi unaozungumziwa, ambao huzalisha chumvi ya mawe (inayotumiwa kutengeneza hidroksidi ya sodiamu na PVC), ni mojawapo ya migodi 35 ambayo kampuni ya Braskem inashughulikia huko Maceio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.