Pata taarifa kuu

Bernardo Arevalo ashinda uchaguzi wa urais nchini Guatemala

Mgombea anayependwa zaidi ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Guatemala siku ya Jumapili, kulingana na hesabu ya Mahakama Kuu ya Uchaguzi (TSE) ikizingatia 95% ya kura zilizopigwa.

Mgombea urais wa chama cha Semilla Bernardo Arevalo afanya mkutano huko Parque Central siku moja baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Guatemala, huko Guatemala City, Guatemala Juni 26, 2023.
Mgombea urais wa chama cha Semilla Bernardo Arevalo afanya mkutano huko Parque Central siku moja baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Guatemala, huko Guatemala City, Guatemala Juni 26, 2023. REUTERS - JOSUE DECAVELE
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi uliyotabiri Arevalo mshindi wa uchaguzi wa rais wa Guatemala hazikudanganya. Mgombea huyo aliyeshtushwa, kwa kukabiliwa na majaribio ya kuenguliwa wakati wa kampeni za uchaguzi, alishinda duru ya pili ya uchaguzi siku ya Jumapili kwa ahadi ya kukomesha ufisadi.

Irma Palencia, rais wa Mahakama ya Juu ya Uchaguzi (TSE), alitangaza kuwa Bernardo Arevalo amepata 59% ya kura baada ya kuhesabiwa kwa 95% ya kura, dhidi ya 36% ya mpinzani wake, mke wa rais wa zamani Sandra Torres. Kura ilifanyika bila "tukio lolote baya" kuripotiwa, TSE ilibaini hapo awali, ikisisitiza bila maelezo zaidi "asilimia ya kihistoria ya kiwango cha ushiriki".

Wapinzani hao wawili, walio naumri wa zaidi ya miaka ya sitini, wote wanadai kuwa wakio katika mrego wa kushoto. Lakini ikiwa rais aliyeshinda uchaguzi anaangazia matumaini ya mabadiliko katika nchi isiyo na usawa, mpinzani wake anachukuliwa kuwa mwakilishi wa shirika hilo. Mkuu wa chama cha Umoja wa Kitaifa wa Matumaini (UNE), Sandra Torres ameahidi programu za usaidizi wa kijamii na ruzuku mbalimbali kwa maskini. Walakini, alipata uungwaji mkono kutoka mrengo wa kulia na wainjilisti na kuzidisha hotuba za kihafidhina. 

  Mke wa zamani wa rais wa zamani wa mrengo wa kushoto Alvaro Colom (2008-2012) anafurahia kuungwa mkono kimya kimya na rais anayemaliza muda wake Alejandro Giammattei, ambaye mamlaka yake yalidhihirishwa na ukandamizaji dhidi ya mahakimu na waandishi wa habari ambao walishutumu rushwa.

Akiwa alishinda kwa mshangao wa kila mtu katika duru ya kwanza, Bernardo Arevalo anaweka matumaini ya mabadiliko, hasa miongoni mwa vijana ambao wanawakilisha 16% ya milioni 9.4 waliosajiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.