Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Brazili: Rais Lula atia saini sheria ya kuzuia upatikanaji wa silaha

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva siku ya Ijumaa alitia saini amri ya kuzuia upatikanaji wa silaha kwa raia, hatu ambayo ilikuwa imewezeshwa na mtangulizi wake Jair Bolsonaro. “Tutaendelea kupambana ili kuwe na silaha chache katika nchi yetu. Ni polisi na jeshi pekee wanaopaswa kuwa na silaha za kutosha,” Lula alisema alipokuwa akiwasilisha mjini Brasilia msururu wa hatua zinazolenga kupunguza ghasia nchini Brazil.

appels
appels © AFP
Matangazo ya kibiashara

Sheria ya kirais ya "udhibiti wa silaha unaowajibika" inapunguza idadi ya silaha zilizoidhinishwa kwa ulinzi wa kibinafsi kutoka nne hadi mbili, na yeyote anayetaka kuzipata atalazimika kuonyesha kwamba anazihitaji sana. Wawindaji, watu wengine wanafanya mazoezi ya silaha, wanaojumuika katika kundi linaloitwa "CACs", sasa wanaweza kumiliki silaha sita pekee, ikilinganishwa na 30 zilizoruhusiwa na sheria ya kirais wakati wa utawala wa Jair Bolsonaro (2019-2022). Uidhinishaji wa kununua risasi pia umewekewa vikwazo kwa kiasi kikubwa.

Amri mpya inaweka kikomo cha saa za kazi kwa mazoezi ya ufyatuaji risasi, na maeneo yake ambayo hayataweza kupatikana tena chini ya kilomita moja kutoka shuleni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.