Pata taarifa kuu

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin azuru Mashariki ya Kati chini ya mvutano

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin aliwasili Jordan siku ya Jumapili kwa ziara ya kikanda ambayo pia itampeleka Misri na Israel. Ziara yake inakuja wakati kunaripotia hali ya mvutano: Mpango wa nyuklia wa Iran unawatia wasiwasi washirika wa Washington na ghasia za mara kwa mara katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu huibua hofu ya kutokea machafuko mabaya zaidi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin. AP - Michael Probst
Matangazo ya kibiashara

Nchini Jordan, Waziri wa Ulinzi wa Marekani alimsikia Mfalme Abdallah akizungumzia "utulivu wa kikanda unaotishiwa" na kuzuka kwa ghasia kwa sasa katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel. Washington inaendelea kuonyesha kutokubaliana na maamuzi na kauli za uchochezi za serikali ya sasa ya mrengo mkali wa kulia nchini Israel.

Wiki iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ilielezea kama "kutowajibika", "kuchukizwa" na matamshi ya Waziri Betzalel Smotrich ambaye alitoa wito wa "kuharibiwa" kwa kijiji cha Wapalestina cha Huwara, kabla ya kukifuta kabisa.

Katika muktadha huu wa machafuko, maafisa wa Marekani wanaendelea kuzuru eneo hilo: baada ya mshauri wa usalama Jake Sullivan na mkuu wa diplomasia Antony Blinken, kwa hiyo ni zamu ya Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin. Pamoja na viongozi wa Israel, atajadili pia mpango wa nyuklia wa Iran, huku Tehran ikikaribia kila mara silaha za atomiki (IAEA inaonyesha kwamba imegundua kiwango cha uranium iliyorutubishwa kwa zaidi ya 83%, ambayo ni kusema karibu sana na ubora wa kijeshi) na kwamba Israeli. inasemekana kupanga kufanya shambulio la mapema dhidi ya mitambo ya nyuklia ya Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.