Pata taarifa kuu

Ujerumani: Olaf Scholz ziarani Amerika Kusini kuimarisha uhusiano

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anaanza Jumamosi hii, Januari 28 ziara ya siku tano Amerika Kusini inayolenga uchumi. Akiwa na viongozi kadhaa wa kampuni, Kansela wa Ujerumani anaenda kwanza Argentina, kisha Chile, kabla ya kumaliza na Brazil.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akipanda ndege ya Airbus A350 Konrad Adenauer, katika sehemu ya kijeshi ya uwanja wa ndege wa Berlin-Brandenburg, Jumamosi hii, Januari 28, 2023, kuelekea Amerika Kusini.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akipanda ndege ya Airbus A350 Konrad Adenauer, katika sehemu ya kijeshi ya uwanja wa ndege wa Berlin-Brandenburg, Jumamosi hii, Januari 28, 2023, kuelekea Amerika Kusini. AP - Kay Nietfeld
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi tatu kubwa za Amerika ya Kusini zinawakilisha soko la takriban wakazi milioni 278. Kwa hivyo zinavutia sana kiuchumi kwa Ujerumani, ambayo imepoteza soko la Urusi kutokana na vita vya Ukraine na ambayo inatafuta kupunguza utegemezi wake mkubwa wa kibiashara kwa China.

Wakati eneo hili ni tajiri sana katika malighafi muhimu, hasa shaba na lithiamu inayoitwa dhahabu mpya nyeupe, ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji wa betri kwa magari ya umeme.

Ziara ya Kansela wa Ujerumani itafanya pia uwezekano wa kuendeleza makubaliano ya biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na MERCOSUR, inayoundwa na Brazil, Argentina, Uruguay na Paraguay. Makubaliano hayo yaliyokamilishwa mnamo 2019, hayakuwahi kupitishwa kwa sababu hasa ya wasiwasi wa Ulaya juu ya sera ya mazingira ya Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro.

Lakini kurejea kwa Lula da Silva Brazil kunaihakikishia Umoja wa Ulaya. Rais wa mrengo wa kushoto, ambaye anajionyesha kama mtetezi wa mazingira, amejitolea kuhifadhi Amazon, mapafu ya sayari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.