Pata taarifa kuu

Macron mjini New Orleans kusherehekea Francophonie

Emmanuel Macron anahitimisha ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini Marekani siku ya Ijumaa kwa kuzuru New Orleans, jiji ambalo ni nembo ya uhusiano wa kihistoria wa Ufaransa na Marekani ambapo ataendeleza na kukuza kukuza Kifaransa kupitia Francophonie.

Marais Emmanuel Macron na Joe Biden wakizungumza katika ofisi ya ikulu ya White House huko Washington, Alhamisi, Desemba 1, 2022.
Marais Emmanuel Macron na Joe Biden wakizungumza katika ofisi ya ikulu ya White House huko Washington, Alhamisi, Desemba 1, 2022. © JEAN-CLAUDE COUTAUSSE POUR LE MONDE
Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya mapokezi ya kifahari katika Ikulu ya White House ambayo yaliashiria "urafiki" wa rais wa Ufaransa na mwenzake wa Marekani Joe Biden, rais wa Ufaransa atafanya saa 24 katika jiji la Louisiana, kusini-mashariki mwa nchi.

"New Orleans" ambayo ilikuwa ni eneo la Ufaransa, liliuzwa nchini Marekani na Napoleon Bonaparte mwaka wa 1803.

"Katika New Orleans, katika ardhi inayozungumza Kifaransa ikiwa ipo", Rais Macron amedokeza kwamba atatangaza mpango "kabambe": mfuko wa 'French For All', kusaidia ujifunzaji wa Kifaransa popote pale nchini Marekani, kuanzia shule ya chekechea hadi chuo kikuu, hasa kwa wraia wenye maisha duni ambao wanaweza kupata kupitia Kifaransa fursa nyingi zaidi", alisema siku ya Jumatano mbele ya wananchi wa Ufaransa waishio Washington.

Aliongeza kuwa anataka kukarabati "taswira ya lugha ya Kifaransa nchini Marekani, ambayo wakati mwingine inaonekana kama ya wasomi".

Baada ya Jenerali de Gaulle mnamo 1960, Emmanuel Macron alichagua kuzuru New Orleans. Hatokosa kutembea katika mitaa ya "NoLa", pengine katika "Vieux Carré", au "French Quarter", kitovu cha kihistoria cha jiji hili, ambalo wakazi wake wengi ni Wamarekani wenye asili ya Afrika.

"Tuna historia huko New Orleans na mambo muhimu ya kusema mara moja ambayo yanahusu historia yetu na kile tunachotaka kufanya kwa siku zijazo," ikulu ya Elysée imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.