Pata taarifa kuu
MEXICO-MAREKANI-HAKI

Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Mexico azuiliwa Marekani

Jenerali Salvador Cienfuegos Zepeda, ambaye alikuwa waziri wa ulinzi wa rais wa zamani wa Mexico Enrique Pena Nieto, amekamatwa huko Los Angeles.

Chanzo cha kidiplomasia cha Mexico kimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu wa familia ya Zepeda, ambao walikuwa wakisafiri naye, tayari wameachiliwa huru.
Chanzo cha kidiplomasia cha Mexico kimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu wa familia ya Zepeda, ambao walikuwa wakisafiri naye, tayari wameachiliwa huru. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo linakuja baada ya shirika la Marekani linalopambana dhidi ya madawa ya kulevya (DEA) kutoa hati ya kukamatwa Kwa jenerali huyo mstaafu, msemaji wa DEA ameliambia shirika la habari la Reuters.

Msemaji wa DEA huko Los Angeles, Nicole Nishida, amesema hana maelezo zaidi ya kuzungumzia kuhusu yaliyomo kwenye hati ya kukamatwa kwa Jenerali Salvador Cienfuegos Zepeda au mazingira ya kukamatwa kwake.

Hata hivyo shirika la habari la Reuters limebaini kwamba limepata taarifa ya kukamatwa kwa Jenerali Salvador Cienfuegos Zepeda kutoka vyanzo vya kidiplomasia nchini Mexico na Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Marcelo Ebrard, almesema Balozi wa Marekani nchini Mexico Christopher Landau alimjulisha juu ya kukamatwa kwa Jenerali Salvador Cienfuegos Zepeda.

"Ubalozi mdogo wa Los Angeles utatufahamisha mashtaka dhidi ya Jenerali Salvador Cienfuegos Zepeda ndani ya saa chache zijazo. Tutatoa msaada wa kibalozi ambao anastahili kupata," Marcelo Ebrard ameongeza kwenye Twitter.

Chanzo cha kidiplomasia cha Mexico kimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu wa familia ya Zepeda, ambao walikuwa wakisafiri naye, tayari wameachiliwa huru.

Wajumbe kadhaa wa serikali na chama cha rais wa zamani Nieto wamehusishwa kwenye mstari wa mbe katika visa vya ufisadi, wengine wakihusishwa katika uhalifu uliopangwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.