Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Donald Trump akataa kushiriki mjadala mbele ya Bunge unaolenga kumng'atua madarakani

Ikulu ya Marekani imesema rais Donald Trump na Mawakili wake, hawatahudhuria kikao kinachoendelea mbele ya bunge, kinacholenga kumwondoa madarakani.

Rais wa Marekani amekataa kushiriki katika mjadala wa Bunge unaolenga kumuondoa madarakani, baada ya kualikwa kuhudhuria kikao hicho. (picha ya kumukumbu).
Rais wa Marekani amekataa kushiriki katika mjadala wa Bunge unaolenga kumuondoa madarakani, baada ya kualikwa kuhudhuria kikao hicho. (picha ya kumukumbu). Joshua Roberts/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kupitia barua iliyowasilishwa kwa kamati inayoshughulia masuala ya sheria bungeni, Ikulu ya Marekani imesema, Trump hatafika mbele ya wabunge hao, kama ilivyokuwa imepangwa siku ya Jumatano.

Hata hivyo, Ikulu ya Marekani haijasema iwapo Trump pia hatahudhuria kikao cha pili ambacho kinatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Trump kupitia barua hiyo, amesema, hawezi kushiriki katika mchakato ambao anasema unaegemea upande mmoja, na ambao hauaminiki.

Rais Trump anachunguzwa na wabunge, kwa madai ya kumjadili aliiyewahi kuwa Makamu wa rais Joe Biden na kiongozi wa Ukraine, na kushinikiza achunguzwe kuhusu madai ya ufisadi.

Katiba ya Marekani haimruhusu rais kumjadili mpinzani wake wa kisiasa katika nchi nyingine kwa maslahi binafasi, madai ambayo Trump ameendelea kukanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.