Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA-HAKI

Nancy Pelosi: Uchunguzi wa kumng'oa Donald Trump waanza

Spika wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha Democratic nchini Marekani Nancy Pelosi ametangaza kwamba uchunguzi kwa mashtaka dhidi ya Donald Trump umeanza rasmi.

Spika wa Baraza la Congress la Marekani Nancy Pelosi.
Spika wa Baraza la Congress la Marekani Nancy Pelosi. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa Marekani anatuhumiwa kuwa alimuomba mwenzake wa Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa Joe Biden kwa madai ya ufisadi.

Wabunge wa Chama cha Democratic wamesema kuwa Trump alijaribu kuitisha nchi Ukraine kuwa hataitolea msaada wa kijeshi iwapo haitamchunguza Biden.

Spika wa bunge ambaye pia ni kiongozi wa juu wa cham cha Democratic Nancy Pelosi, amesema rais Trump ni lazima awajibike.

"Vitendo vya rais hadi leo vimevunja Katiba, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani kutoka chama cha Democratic Nancy Pelosi amebaini. Leo, natangaza kwamba Baraza la Wawakilishi linaanzisha uchunguzi rasmi kuhusu mchakato wa kumng'oa madarakani Donald Trump. "

Hii ni hatua ya kwanza katika mashtaka ya kumng'atua madarakani rais wa Marekani, ambaye Baraza la Wawakilishi linamshutumu kwa kufanya matumizi mabaya ya madaraka. Nancy Pelosi, ambaye kwa miezi mingi alikataa kutumia njia hiyo, hatimaye amekubali kushirikiana na wengine kwa kuomtimua Donald Trump madarakani.

Suala la Ukraine lazua sintofahamu

Kesi hii ya simu kati ya Donald Trump na mwenzake wa Ukraine, ambayo maudhui yake yatajulikana leo Jumatano, inasubiriwa kwa hamu na gamu nchini Marekani. Spika wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani anada pia kujua yaliyomo katika malalamiko yaliyowasilishwa na mtu aliyetiwa wasiwasi kuhusu hatua za rais.

Baraza la Wawakilishi litachunguza ikiwa Donald Trump alitafuta msaada kutoka Ukraine ili kupata taarifa inayoweza kumuweka matatani Joe Biden, ambaye anapewa nafasi kubwa katika kinyang'anyiro cha kumteuwa mgombea kutoka chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 nchini Marekani.

Rais anapaswa kujibu. Hakuna mtu aliye juu ya sheria, "amesema Nancy Pelosi. Saa chache kabla, Joe Biden ameonyesha msimamo wa kumng'oa madarakani rais Donald Trump.

"Ni wakati wa serikali kuacha kuweka kizuizi na kulipa nafasi Baraza la Wawakilishi kupata ukweli wote, ikiwa ni pamoja na nakala ya malalamiko ya mtu aliyetiwa wasiwasi na hayua hizo za rais," amesema Joe Biden. Na ni wakati wa Baraza la Congress kuchunguza kabisa mwenendo wa rais huyo. Rais aache kuweka kizuizi kwenye uchunguzi huo na uchunguzi mwingine wowote katika utekelezwaji wake hatua zake mbovu, " ameongeza Joe Biden.

Muda mfupi baada ya tangazo la Nancy Pelosi, timu ya rais imetuma ujumbe mfupi unaotoa wito wa kutoa michango ili kufadhili upande wa utetezi wa Donald Trump, kwa mujibu wa mwandishi wa wetu Wahsington, Anne Corpet.

Rais Trump hata hvyo, kwenye ukurasa wake wa Twitter, amepuuzilia mbali harakati za wabunge wa Democratic na kusema hatua hiyo itamsaidia kushinda Uchaguzi mwaka ujao.

Utaratibu wa kumg'oa rais madarakani unafanyika kwa hatua kadhaa. Baraza la Wawakilishi linachunguza na, ikiwa ni lazima, linaandika na kupiga kura kwa wingi wa sauti kuhusu kumfungulia mashitaka rais. Ikiwa Baraza la wawakilishi litapiga kura ya kumg'oa rais madarakani, hatua inayofuata ni Bunge la Seneti kuanda kesi. Uamuzi wa kumuweka rais hatiani hupitishwa na iwingi wa theluthi mbili.

Joe Biden ni miongon mwa viongozi wa juu wa chama cha Democratic ambao wametangaza kuwania urais nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.