VENEZUELA-SIASA-UCHUMI
Maduro atangaza mgawo wa umeme kwa siku 30
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ametangaza siku 30 za mgawo wa umeme. Venezuela imeenelea kukabiliwa na uhaba wa umeme kufuatia kutwa kwa Nishati hiyo ya umeme.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Aidha, amesema muda wa kufanya kazi unapunguzwa na shule zitaendelea kufungwa kwa sababu ya ukosefu wa nguvu za umeme katika taifa hilo.
Hata hivyo, ameahidi kuwa serikali yake itahakisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji.
Serikali ya Maduro imeendelea kukumbwa na mzozo wa kiuchumi na kisiasa, huku Marekani ikimwekea rais Maduro vikwazo na kutomtambua kama kiongozi wa nchi hiyo.