Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-UGAIDI

Rais Trump alaani waliotupa vifaa vya mlipuko kwa marais wa zamani

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema usalama wa taifa lake ni jambo alilolipa kipaumbele cha kwanza, matamshi anayotoa saa chache baada ya maofisa usalama kubaini vifaa vya mlipuko vilivyotumwa kwa marais wa zamani na watu mashuhuri.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump ©REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Jumla ya vifurushi vitano vinavyodaiwa kuwa ni mlipuko vilitumwa kwa aliyekuwa mgombea wa chama cha Democratic, Hilary Clinton, rais wa zamani Barack Obama na ofisi za shirika la habari la CNN.

Rais Trump sasa anataka wahusika kusakwa ambapo ametoa wito wa umoja na kuachana na siasa za chuki na vitisho.

Maafisa wa usalama nchini Marekani wanachunguza, waliotuma vilipuzi hivyo na nia yao.

Marekani linasalia taifa linalolengwa na magaidi, hasa viongozi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.