Pata taarifa kuu
MAREKANI-SAUDI ARABIA-MWANAHABARI

Saudi Arabia yapata shinikizo kueleza hatima ya Mwanahabari Jamal Khashoggi

Shinikizo kutoka mataifa ya Magharibi zinaendelea kutolewa kwa serikali ya Saudi Arabia, kueleza hatima ya mwandishi wake Habari Jamal Khashoggi, aliyeaminiwa kuwa aliuawa mikononi mwa maafisa wa Saudia alipotembelea Ubalozi wake jijini Instabul nchini Uturuki.

Jamal Khashoggi Mwanahabari wa Saudi Arabia
Jamal Khashoggi Mwanahabari wa Saudi Arabia MOHAMMED AL-SHAIKH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Khashoggi, alionekana mara ya mwisho wa Ubalozi wa nchi yake wiki mbili zilizopita na haifahamiki yuko wapi.

Uturuki imesema ina uhakika kuwa, Khashoggi aliuawa na maafisa wa Saudi Arabia kwa sababu za makala alizokuwa anaandika kuukashifu uongozi wa Mfalme Salman.

Usiku wa kuamkia siku ya Jumanne, wachunguzi wa Uturuki waliruhusiwa kuingia ndani ya Ubalozi wa Saudi Arabia kabla kufanya uchunguzi wao.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, yupo jijini Riyadh kukutana na Mfalme Salman kuhusu hatima ya mwanahabari huyo.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amezungumza na Mfalme Salman ambaye amekanusha madai ya kufahamu kuhusu kuuawa kwa Mwanahabari huyo ambaye alikuwa mkaazi wa Marekani.

“Nimezungumza na Mfalme Salman, amekanusha kabisa kufahamu lolote, amesema hafahamu lolote,” amesema.

"Lakini tutachunguza kwa kina ili kufahamu ukweli uko wapi," aliongeza.

Ripoti zinasema kuwa, Saudi Arabia inatarajiwa kutoa ripoti kukiri kuwa Mwanahabari huyo aliyekuwa anaandika makala za kuukosoa uongozi wake, alipoteza maisha kwa bahati mbaya akihojiwa wiki mbili zilizopita kwenye Ubalozi wa nchi yake jijini Instanbul.

Saudi Arabia imekuwa ikisema haikuhusika na kifo cha Mwanahabari huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.