Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-NYUKLIA-USALAMA

Marekani yajitoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuiitoa nchi yake katika mkataba wa kimataifa wa mpango wa Nyuklia wa Iran. Ameutaja mpango huo kuwa si salama kwa Marekani na raia wake, huku akisema kuwa mpango huo ni kero kwa taifa la Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump ajitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran.
Rais wa Marekani Donald Trump ajitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Licha ya wito kutoka jumuiya ya kimataifa, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, Donald Trump ametangaza kujitoa kwenye mkataba wa Vienna, uliyosainiwa mwaka 2015 kati ya kundi "5 1" na Iran.

Donald Trump amesema mpango huo hauwezi kuleta amani na usalama hata kama Iran ikikubaliana na kila kitu kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo uliosainiwa mwaka 2015 chini ya utawala wa aliyekuwa rais taifa hilo Barack Obama.

Nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Israel na Saudi Arabia wamepongeza hatu hiyo ya rais wa Marekani.

Makubaliano hayo yanaondoa vikwazo dhidi ya Iran kwa kubadilishana na ahadi kuhusu mpango wake wa nyuklia. Donald Trump mara kwa mara amekua akirejelea kauli yake hiyo ya kujitoa kwenye mkataba huo. Amesma mpango huo wa hatua za pamoja kuwa ni "mbaya." Anaona kuwa mpango huo ni "mbaya zaidi" kuwahi kujadiliwa na Marekani.

Robert Malley, afisa wa marekani aliyeiwakilisha nchi hiyo katika mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran wakati wa utawala wa Barack Obama, amesema kujiondoa kwa Marekani kwenye mkataba huo, kuna hatari ya kuongezeka kwa mvutano kati ya Marekani na Iran, kuna uwezekano wa Iran kujejelea mpango wake wa nyuklia na uwezekano wa makabiliano ya kijeshi kati ya nchi hizi mbili.

"Madhara makubwa, yatajitokeza katika siku, wiki na miezi, na pengine miaka ijayo na kuongezeka kwa mvutano kati ya Marekani na Iran, " amesema Robert Malley, mkurugenzi wa shirika la International Crisis Group na mshauri wa zamani wa Barack Obama kuhusu Ghuba ya Uajemi.

Rais wa Iran amekosoa hatua ya Marekani kujitoa na kudai kuwa haiheshimu makubaliano yake. Hata hivyo Donald Trump amesema kuwa watarejhesha vikwazo vya kiuchumi vilivyoondolewa dhidi ya Iran kupitia makubaliano hayo ya mwaka 2015.

Pitia habari hii: Marekani "itajuta" ikiwa itakiuka makubaliano ya nyuklia ya Iran

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.