Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA

Trump: Hivi karibuni tutaondoa wanajeshi wetu Syria

Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kuwa nchi yake itaondoa vikosi vyake nchini Syria hivi karibuni huku akilaumu kile alichosema ni hatua ya Serikali kupoteza kiasi cha dola za Marekani trilioni 7 kwenye vita vya mashariki ya kati.

Rais wa Marekani akihutubia wafanyakazi wa viwanda mjini Richfield, Ohia, ambapo ametangaza kuwa ataondoa wanajeshi wake Syria, Machi 29, 2018.
Rais wa Marekani akihutubia wafanyakazi wa viwanda mjini Richfield, Ohia, ambapo ametangaza kuwa ataondoa wanajeshi wake Syria, Machi 29, 2018. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kwa wafanyakazi wa viwanda mjini Ohio, Trump amesema vikosi vya Marekani vinakaribia kuchukua maeneo yote ambayo yalikuwa ni ngome ya kundi la islamic State.

“Tutaondoka Syria mapema sana. Tuwaache watu wengine washughulikie suala hilo sasa,” alisema rais Trump.

Trumo hata hivyo hakusema ni akina nani aliokuwa akimaanisha ‘wengine’ ambao watashughulikia mzozo wa syria, lakini inavyonekana ni Iran na Urusi ambazo zinamuunga mkono rais wa Syria Bashar al-Assad.

“Mapema sana, mapema sana tutaondoka. Tutakuwa na asilimia 100 ya umiliki wa maeneo ya Caliphate kama wanavyoiita, tutayachukua haraka sana, hara,” alisema.

Hata hivyo msemaji wa ikulu ya Marekani Heather Nauert alipoulizwa na wanahabari ikiwa anataarifa zozote za kuanza kuondolewa kwa wanajeshi wao nchini Syria alijibu “hapana”.

Nchi ya Marekani inawanajeshi zaidi ya elfu 2 mashariki mwa nchi ya Syria wanaofanya kazi na wapiganaji wazawa kulitokomeza kundi la islamic State.

Uamuzi wa Trump utaenda kinyume na kile ambacho aliyelkuwa waziri wa mambo ya kigeni Rex Tillerson ambaye kwa sasa amefutwa kazi, kudai kuwa vikosi vya Marekani ni lazima visalie nchini Syria kuzuia makundi ya Islamic State na Al-Qaeda kuenea na kuinyima nafasi Iran kufadhili makundi ya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.