Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP

Republicans wamuonya rais Trump kuhusu kuingilia uchunguzi wa Mueller

Rais wa Marekani Donald Trump ameonywa na viongozi wenzake kutoka chama cha Republican kuhusu kuingilia kazi zinazofanywa na Robert Mueller anayeongoza jopo la uchunguzi ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Rais wa Marekani, Donald Trump.
Rais wa Marekani, Donald Trump. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limetolewa baada ya rais Trump kumshambulia Mueller kuhusu uchunguzi wake ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Katika mtandao wake wa kijamii wa twitter rais Trump amesisitiza kuwa hakukuwa na ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trumo na Urusim ambapo ameita uchunguzu wa Mueller kama wa kutafuta mchawi.

Rais Trump ameongeza kuwa timu ya uchunguzi ya Mueller imesheheni watu kutoka chama cha Democrats.

Mueller mwenyewe ambaye wakati fulani alisifika kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi la FBI, ni mwanachama wa chama cha Republican.

Mkuu wa jopo la uchunguzi Marekani Robert Mueller anayechunguza ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi wa mwaka 2016
Mkuu wa jopo la uchunguzi Marekani Robert Mueller anayechunguza ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi wa mwaka 2016 Reuters/路透社

Seneta wa chama cha Republican Lindsey Graham amesema kuwa Mueller anapaswa kupewa nafasi ya kuendelea na kazi bila kuingiliwa wazo ambalo limeungwa mkono na viongozi wengine wa Republican.

Seneta huyo amemuonya pia rais Trump dhidi ya njama zozote za kutaka kumfuta kazi Mueller na timu yake.

"Kama atajaribu kufanya hivyo huo huenda ukawa ndio mwisho wa utawala wake, kwasababu sisi ni nchi ya utawala wa sheria," alisema Graham.

Seneta mwingine wa Republican Jeff Flake ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Trump amesema matamshi yake ya hivi sasa ni wazi yanaandaa mpango wa kumfuta kazi Mueller.

Kwa upande wake kiongozi wa chama cha Democrats kwenye Seneti Charles Schumer amemtuhumu rais Trump kwa kujaribu kuingilia uchunguzi wa Mueller.

Matamshi ya rais Trump yamekuja siku moja tu baada ya wakili wake John Dowd kusema kuwa ni muda uchunguzi wa Mueller umalizike. Awali wakili huyu alisema anazungumza kwa niaba ya Trump lakini baadae akabadili matamshi yake na kudai yalikuwa ni maoni yake binafsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.