Pata taarifa kuu
PERU

Rais wa Peru ashinda kura ya kutokuwa na imani nae bungeni

Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski amefanikiwa kusalia madarakani baada ya kushinda kura ya kutaka kumuondoa madarakani iliyoitishwa na wabunge wakimtuhumu kwa rushwa na uhusiano aliokuwa nao na mfanyabiashara maarufu wa ujenzi raia wa Brazil.

Rais wa Peru, Pérou Pedro Pablo Kuczynski.
Rais wa Peru, Pérou Pedro Pablo Kuczynski. REUTERS/Mariana Bazo
Matangazo ya kibiashara

Spika wa bunge la Peru Luis Galarreta akitangaza matokeo ya kura hiyo, aliwaambia wabunge kuwa idadi ya kura zilizotakiwa kumuondoa madarakani rais Kuczynski hazikutimia.

Wabunge 79 waliunga mkono rais Kuczynski kuondoka madarakani huku 19 wakiupinga na 21 hawakuhudhuria kikao cha bunge.

Kura hiyo ilishindwa kwa kura 8 zilizokuwa zinatakiwa kufikia idadi ya 87 zilizohitajika kumuondoa madarakani rais Kuczynski.

Kupitia kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter rais Kuczynski amewataka wananchi kua na imani nae huku akisisitiza kurejea kwa shughuli zake za kawaida kuijenga nchi hiyo.

Awali rais Kuczynski aliutaja uamuzi huo wa wabunge kutaka kumng’oa madarakani ulikuwa ni jaribio la mapinduzi na mashambulizi dhidi ya Demokrasia.

Wadadisi wa mambo walitabiri kuwa huenda rais Kuczynski angeanguka kwenye kura hiyo kutokana na matokeo ya awali wakati wa kupitisha upigwaji wa kura hiyo, wabunge 93 kuiunga mkono.

Kuczynski alikuwa anatuhumiwa kupokea kiasi cha dola za Marekani milioni 5 kutoka kwa kampuni ya ujenzi ya Odebrecht ya Brazil akisisitiza malipo hayo yalikuwa halali kutokana na kazi iliyofanyika.

Pesa hizo anadaiwa kuzipokea kati ya mwaka 2004 na 2013 wakati Kuczynski akiwa waziri wa fedha na mkuu wa baraza la mawaziri la aliyekuwa rais wakati huo, Alejandro Toledo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.