Pata taarifa kuu
BRAZIL-HAKI

Rais wa Brazil afunguliwa mashitaka ya rushwa

Rais Temer wa Brazil anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu. Rais Temer amefunguliwa mashitaka kwa kosa la kuzuia sheria kuchukuwa mkondo wake na kuhusika katika mtandao wa rushwa.

Rais wa Brazil Michel Temer akabiliwa na mashtika ya rushwa.
Rais wa Brazil Michel Temer akabiliwa na mashtika ya rushwa. Ricardo Botelho/Brazil Photo Press/LatinContent/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Rais Temer anashtumiwa kuchukua hongo na kujaribu kuwanyamazisha mashahidi.

Hata hivyo Bw. Temer amepinga madai hayo na kusema kwamba yanalenga kumuangusha madarakani.

Hatua hiyo ni ya pili katika kesi ya jinai inayomkabili rais Temer.

Bunge la uwakilishi lilizuia mashtaka ya awali ya ufisadi. Itafahamika kwamba bunge hilo lina uwezo wa kuamua iwapo rais anafaa kufunguliwa mashtaka au la.

Mwendesha mashtaka wa kesi za ufisadi nchini Brazil amemfungulia mashtaka rais Michel Temer kwa kosa la kuzuia sheria kuchukuwa mkondo wake na na kujaribu kuwanyamazisha mashahidi.

Kiongozi wa mashtaka Rodrigo Janot alisema katika taarifa kwamba bwana Temer alihudumu kama kiongozi wa genge la wahalifu linaloshirikisha wanachama waandamizi wa chama chake cha PMDB.

Mashtaka hayo yanatokana na ushahidi uliotolewa na mmiliki wa kampuni kubwa ya nyama JBS Joesely Batista na Wesley Batista.

Bw. Janot mesema kuwa kundi hilo lilidaiwa kuchukua hongo ya takriban dola milioni 190 kwa lengo la kuwazawadi waliotoa fedha hizo kandarasi katika kampuni za umma.

Katika shtaka la pili rais Temer ameshtakiwa pamoja na washirika wake sita wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.