Pata taarifa kuu
HAITI-UNSC-USHIRIKIANO

Ujumbe wa UNSC wapokelewa shingo upande nchini Haiti

Wawakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanazuru Haiti, katika ziara ya masaa 48 ili kutathmini hali inayojiri katika nchi hii kabla ya kuondoa tume ya Umoja wa Mataifa (Minustah) iliyotumwa nchini humo tangu 2004.

Waandamanaji mia mbili waandamana maeneo ya jirani ya majengo ya Ministah, makao makuu ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti, Juni 22, 2017.
Waandamanaji mia mbili waandamana maeneo ya jirani ya majengo ya Ministah, makao makuu ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti, Juni 22, 2017. HECTOR RETAMAL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa haujakaribishwa vizuri.

Rais wa Haiti na Serikali yake wamewapokea wajumbe wa baraza hilo baada ya dakika 40 ya kuchelewa, wakati ambapo watu 200 walikua wakiandamana nje ya makao makuu ya tume ya Umoja wa Matiafa nchini Haiti (Minustah) katika mji wa Port-au-Prince. Haiti inalaumu kikosi cha Umoja wa mataifa nchini humo kuleta maradhi ya kipindupindu mwaka 2010 ugonjwa ambao tayari umewaua watu 9,000.

Waandamanaji hawa 200, wamekua wamekua na mabango yalioandikwa Minustah daima itaendelea kukabilwa na kipindupindu. Miaka saba baada ya kuibuka kwa janga hilo, waandamanaji hao wanalalamika wakionyesha hasira yao kwa ukosefu wa huduma ya Umoja wa Mataifa.

Fedha zakosekana

Kwa ssasa fedha zimekosekana kwa kuwahudumia raia wa Haiti. Kwa jumla ya Dola Milioni 400 zinazohitajika, milioni 2.7 tu ndio zimekusanywa tangu mwezi Desemba 2016. Sacha Sergio Llorenty Soliz, mwakilishi wa Bolivia kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, amesem ahawezi kupinga ukweli huu: "Tunatambua kwamba kuna tatizo na tuko hapa kuanzisha upya ahadi ya Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na tatizo hili na kulikulitafutia suluhu. "

Tukio jpya

Waathirika wa kipindupindu wamepanga kuandamana tena Ijumaa hii, karibu na eneo ambapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana na wajumbe wa mashirika ya kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.