Pata taarifa kuu
MAREKANI

Rais Trump akerwa na ripoti kuwa anachunguzwa

Rais wa Marekani amekasirishwa na ripoti kuwa anachunguzwa kwa madai ya kuzuia haki pamoja na hatua ya kumfuta kazi aliyekuwa Mkuu wa FBI James Comey.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Trump amesema kinachoendelea ni kuandamwa kisiasa na watu ambao amesema ni wabaya.

“Mnashuhudia uwindwaji wa aina yake katika historia ya kisiasa nchini Marekani, unaoongozwa na watu wabaya,” amesema Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Trump amekuwa akikabiliwa na changamoto mbalimbali tangu alipoapishwa kuwa rais mwezi Januari ikiwa ni pamoja na kumfuta kazi aliyekuwa mkuu wa FBI James Comey.

Aidha, baada ya kumfuta kazi aliyekuwa mshauri wake wa maswala ya usalama Michael Flynn, kwa madai kuwa alishirikiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita, Trump anadaiwa kuzuia kuchunguzwa kwake.

Comey akihojiwa na Kamati ya Senate wiki hii, alisema anaamini Urusi iliingilia Uchaguzi wa Marekani.

Madai haya yamekanushwa na Trump na washirika wake pamoja na serikali ya Urusi.

Shirika la FBI limemteua mchunguzi maalum Robert Mueller, kkubaini ukweli wa madai haya huku makamu wa rais Mike Pence akimteau wakili maarufu Richard Cullen kumwakilisha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.