Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USALAMA

Jeff Sessions akanusha tuhuma dhidi yake

Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Marekani Jeff Sessions amekanusha vikali madai kuwa alishirikiana na maofisa wa Urusi walioingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana na kumsaidia rais Donald Trump kuchaguliwa.

Mwanasheria mkuu wa serikali ya Marekani Jeff Sessions, wakati akihojiwa na bunge la Seneti, Washington, Juni 13, 2017.
Mwanasheria mkuu wa serikali ya Marekani Jeff Sessions, wakati akihojiwa na bunge la Seneti, Washington, Juni 13, 2017. REUTERS/Aaron P. Bernstein
Matangazo ya kibiashara

Jeff sessions alihojiwa na bunge la Seneti siku ya Jumanne kwa muda wa saa karibu tatu katika uchunguzi wa Urusi. Bw sessions, kwa mara nyingi, alisema uaminifu wake, na kufutilia mbali madai yoyote ya kula njama na Urusi. Jeff Sessions, mara nyingi alikataa kujibu maswali ya maseneta.

Siri inayozunguka uchunguzi wa Urusi haikuweza kufichuliwa. Mwanasheria mkuu wa serikali ya Marekani alijiondoa mwenyewe juu ya suala hili. Amesema kuwa kujiondoa si kukiri kosa: "Sitaki kuzungumza lolote hapa ili ionekani kuwa siri nilivujisha sri ya majukumu yangu, mimi sipendelei hivyo! Nitajaribu kufanya ninachokiweza ili kutoa majibu mazuri. Watu wanadai kwamba mimi si mwaaminifu juu ya mambo fulani, lakini ninajaribu kuwa mwaaminifu. "

Jeff Sessions amethibitisha wasiwasi wa alie kuwa mkurugenzi wa shirikala ujasusi la FBI, James Comey. Ndiyo, mkurugenzi wa FBI alimuomba kutomwacha peke yake na rais. Lakini, James Comey hakukumpa maelezo zaidi.

Akiulizwa kuhusu mchango wake katika kufukuzwa kwa mkurugenzi wa FBI, swali hili lilimkera Jeff Sessions. Mara nyingi, Jeff Sessions alikataa kuzungumza, akiongelea siri ya mazungumzo na rais. Na maswali mengi hayakujibiwa kwa sababu Jeff Sessions alisem akuwa hayakumbuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.