Pata taarifa kuu
ISRAEL-PERU-SHERIA

Israel kutompokea rais wa zamani wa Peru Toledo

Israel imetangaza Jumapili hii kwamba haitompokea kwenye ardhi yake rais wa zamani wa Peru Alejandro Toledo, anayetafutwa na mahakama ya nchi yake kwa kosa la rushwa.

Alejandro Toledo, Washington, 17 Juni 2016. Rais wa zamani wa Peru atafutawa na mahakama ya Peru kwa kosa la rushwa, akituhumiwa kupokea mamilioni ya dola kutokakampuni ya ujenzi ya Brazil ya BTP Odebrecht.
Alejandro Toledo, Washington, 17 Juni 2016. Rais wa zamani wa Peru atafutawa na mahakama ya Peru kwa kosa la rushwa, akituhumiwa kupokea mamilioni ya dola kutokakampuni ya ujenzi ya Brazil ya BTP Odebrecht. Mandel Ngan / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Bw Toledo ataruhusiwa (kuingia) katika kardi ya Israel pale tu kesi yake itakua imeshughulikia na vyombo vya sheria vya nchi yake," Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel, Emmanuel Nahshon.

Serikali ya Peru ilisema Ijumaa Februari 10 kwamba ina taarifa kwamba rais wa zamani wa Peru, ambaye mkewe ni raia wa Israel, amekua akijaribu kukimbilia nchini Israeli. Awali alikua kitaka kukimbilia katika mji wa Paris nchini Ufaransa.

Viongozi wa nchi zote mbili walionywa, taarifa hiyo imebaini.

Bw Toledo, bingwa wa mapambano dhidi ya rushwa, anashtumiwa kwamba alipokea milioni 20 kutoka kwa kampuni kubwa ya ujenzi ya Brazil ya BTP Odebrecht kwa minajili ya kushinda zabuni kwa ujenzi wa barabara kuu inayounganisha Peru na Brazil.

Rais wa zamani amekanusha madai hayo, akilaani kuwa anafuatiliwa kutokana na mzozo wa kisiasa.

Alhamisi Februari 9, Jaji Richard Concepcion, anayeshughulikia kesi hiyo, alitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa, akiagiza kukamatwa na kufungwa mara moja rais wa zamani wa Peru (kuanzia mwaka 2001 hadi 2006). Jaji huyo pia aliagiza kupewa kifungo cha muda cha miezi 18.

Serikali ya Peru imetoa Dola 30,000 kwa malipo ya mtu atakayetoa taarifa kuhusu sehemu aliko rais huyo wa zamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.