Pata taarifa kuu
MEXICO

Polisi nchini Mexico wawatawanya waandamanaji kwa mabomu ya machozi

Polisi nchini Mexico wametumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji wanaopinga ajenda za mabadiliko zilizopendekezwa na Rais wa nchi hiyo Pena Nieto.Rais Pena Nieto alitarajiwa kuhutubia umma siku ya jana jumapili lakini ratiba hiyo iliahirishwa mpaka leo kutokana na sababu za kiusalama.

RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Mwishoni mwa juma maelfu ya wanafunzi waliungana na walimu wao walioongoza maandamano kadhaa katika mji mkuu wa nchi hiyo katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita wakipinga mapendekezo ya mabadiliko katika sekta ya elimu.

Taarifa kutoka Idara ya usalama zinasema watu wanne wanashikiliwa wakituhumiwa kuchochea ghasia hizo ambazo kwa upande mwingine zinapinga mpango wa serikali kutaka kubinafsisha sekta ya nishati kwa wawekezaji wa kigeni.

Walimu wapatao 10,000 wameendelea kupiga kambi katika uwanja wa Zocalo hatua iliyopelekea kuathiriwa kwa baadhi ya safari za ndege na kuahirishwa kwa michezo miwili ya soka iliyokuwa imepangwa kufanyika mjini hapo.

Tayari bunge limekwishapitisha baadhi ya mabadiliko katika sekta ya elimu na wanatarajia kupigia kura pendekezo la sheria mpya itakayowalazimu walimu kufanya usahili kabla ya kuajiriwa au kupandishwa vyeo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.