Pata taarifa kuu
MEXICO

Mshindi wa Pili wa Uchaguzi wa Rais nchini Mexico ataka kura zihesabiwe upya

Mshindi wa Pili kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais nchini Mexico Andres Manuel Lopez Obrador ametaka Tume Huru ya uchaguzi nchini humo irejee tena kuhesabu kura akidai uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Mshindi wa Pili wa Uchaguzi wa Rais nchini Mexico Andres Manuel Lopez Obrador akihutubia wafuasi wake
Mshindi wa Pili wa Uchaguzi wa Rais nchini Mexico Andres Manuel Lopez Obrador akihutubia wafuasi wake
Matangazo ya kibiashara

Manuel Lopez Obrador amesema uchaguzi huo haukuendeshwa kwa uwazi kitu ambacho kinaweza kikaibua maandamano makubwa katika nchi hiyo kama yale ambayo yalishuhudiwa miaka sita yaliyopita baada ya uchaguzi wa rais.

Mshindwa huyo kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa rais kilichofanyika siku ya jumapili amesema mshindi aliyetangazwa Enrique Pena Nieto hakushinda kihalali kwenye uchaguzi huo.

Mgombea huyo kutoka mrengo wa kushoto amesema Pena Nieto ameshinda uchaguzi huo wa rais kutokana na kununua kura za mamilioni ya wapigakura lakini hakushinda kihalali kama ambavyo anajigamba.

Manuel Lopez Obrador amesema iwapo Tume Huru ya uchaguzi itashindwa kuhesabu upya kura ni wazi kile ambacho kilitokea mwaka 2006 na sita kitarejea upya na wananchi wanaandamana kupinga matokeo hayo.

Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni za mrengo wa kushoto Ricardo Monreal akiwa ameambatana na Manuel Lopez Obrador amesema wanaushaidi kuna kura laki moja na elfu thelathini ambazo ziliwekwa kwenye visanduku vya kupigia kura.

Matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi nchini Mexico yalimpa ushindi wa asilimia thelathini na nane mgombea kutoka Chama Cha PRI Pena Nieto huku nafasi ya pili ikienda kwa mgombea wa Chama Cha PRD Manuel Lopez Obrador aliyeambulia asilimia thelathini na moja tu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.