Pata taarifa kuu
Chile

Rais wa Chile awambia hakuna cha bure wanafunzi wanaoandama

Serikali ya Chile imeyakataa na kuyapuuza madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaoandamana kuishinikiza Serikali iweke mfumo wa elimu ya vyuo vikuu bure kwa wote nchini humo.

© Gobierno de Chile
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Chile Sebastian Pinera amesema kuwa katika maisha ya sasa hakuna na cha bure na kila mmoja anawajipika kulipia huduma na mahitaji mengine anayopata.

Rais huyo amesema kuwa kila raia angehitaji huduma ya elimu, huduma za afya na huduma nyingine za jamii bila malipo lakini haiwezekani na vigumu kuwa na mfumo kama huo.

Amesema kama Serikali yake itatoa elimu ya bure kwa asilimia kumi ya wananchi wake basi itakuwa ni sawa kuwakata kodi wananchi wote hususan masikini ambao ni wahitaji wakubwa.

Mpango wa elimu bila malipo imekuwa ni hitaji kubwa la waandamanaji hao huku wakifanya maandamano ya mara kwa mara baada ya Rais Pinera kutangaza mpango wa kubana matumizi katika sekta ya elimu miezi miwili iliyopita.

Katika hatua nyingine vyama vya wafanyakazi wa sekta ya umma na migodi wamesema wataungana na wanafunzi hao kudai haki na maandamano hayo yameshusha umaarufu wa Rais huyo kwa asilimia 26.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.