Pata taarifa kuu

Ongezeko la joto duniani: Nusu ya watu duniani "wako hatarini", yasema IPCC

Ripoti mpya ya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu madhara ya mababadiliko ya tabia nchi, inaonesha kuwa, asilimia 14 ya viumbe hai vipo katika hatari ya kutoweka kwenye uso wa dunia, kufuatia ongezeko la kiwango cha joto. 

Nchini Afghanistan, mwishoni mwa mwaka 2021, ukame mkali ulilazimisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao na kuishi katika umaskini uliokithiri.
Nchini Afghanistan, mwishoni mwa mwaka 2021, ukame mkali ulilazimisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao na kuishi katika umaskini uliokithiri. AP - Mstyslav Chernov
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia kiwango cha joto kuongezeka kwa Sentigredi 1.5, ripot hiyo iliyotolewa na wataalam wa mazingira inaonya kuwa, hali itakuwa mbaya iwapo uhifadhi wa mazingira hautafanyika angalau kwa asililia 30 au 50. 

Iwapo hali itasalia kuwa kama ilivyo na kiwango cha joto kuongezeka kwa nyuzi joto mbili au tatu, basi asilimia 18 ya viumbe hai vitatoweka duniani kwa mujibu wa ripoti hiyo. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewataka viongozi wa dunia kuweka maneno yao kwa vitendo na kuwashtumu kwa kutowajibikia majukumu yao ya kupambana na mabadililiko ya tabia nchi. 

Aidha, amesema nusu ya watu duniani maisha yao yapo hatarini, suala ambalo linapaswa kupewa uzito na viongozi wa dunia. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.