Pata taarifa kuu
DUNIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vya maambukizi vyapindukia zaidi ya Milioni 22 duniani

Zaidi ya watu milioni 22 wameambukizwa virusi vya Corona ulimwenguni, kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins, huku watu 781, 078 wakithibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Mlipuko wa virus vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.
Mlipuko wa virus vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019. Arsene Mpiana / AFP
Matangazo ya kibiashara

Marekani imeorodheshwa taifa lenye idadi kubwa ya maambukizi, ikifuatiwa na Brazil, India, Urusi na Afrika Kusini.

Afrika Kusini ndio inaongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi barani Afrika.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.