Pata taarifa kuu
DUNIA-WHO-CORONA-AFYA

WHO yaonya serikali kuchukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi vya Corona

Watu zaidi ya Milioni 13 sasa wameambukizwa virusi vya Corona duniani, wakati huu Shirika la Afya Duniani, WHO, likiendelea kusema hali inaendelea kuwa mbaya.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo. Fabrice Coffrini/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani, nchi ya Marekani inaongoza kwa maambukizi zaidi ya Milioni tatu, ikifutwa na Brazil, India, Urusi na Peru.

Marekani imeshuhudia ongezeko la maambukizi wakati kukiwa na mvutano kati ya wataalamu wa afya na Rais Donald Trump.

Marekani imerekodi vifo zaidi ya 135,000 kwa mujibu wa Chuo cha Johns Hopkins.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo.

Janga la corona litakuwa ''baya na baya zaidi'' ikiwa serikali zitashindwa kuchukua hatua madhubuti, Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.