Pata taarifa kuu
CAR-EBOLA-AFYA

Virusi vya Ebola: Maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati watiwa hofu

Waziri wa Afya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Pierre Somse, amesema nchi yake haijajiandaa ikiwa kutatokea maambukizi ya virusi hatari vya Ebola ambavyo vinasumbua nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo watu elfu 1,700 wamepoteza maisha mpaka sasa kutokana na ugonjwa huo.

Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018.
Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ya kukubali ukweli kuwa haijajiandaa ikiwa kutaripotiwa maambukizi, imekuja ikiwa ni wiki moja tu imepita tangu shirika la Afya Duniani (WHO) liutangaze ugonjwa wa Ebola nchini DRC kama janga la kidunia.

Hakuna mgonjwa yeyote wa Ebola aliyeripotiwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini changamoto za kiuchumi na muingiliano wa watu vinazidisha hatari ya uwezekano wa kuzuka kwa maradhi hayo hatari.

Waziri Somse, amesema raia wao wanauziana wanyama na majirani, zaidi walioko nchini DRC, huku makundi ya waasi yanayotatiza usalama nchini humo yakivuka mpaka wa nchi hizo mbili mara kwa mara.

Mwakilishi wa shirika la Afya Dunia (WHO) nchini Jamhiri ya Afrika ya Kati, Severin Von Xylander, amesema kuwa nchi hiyo kuwa na uwezo wa kukabiliana na maambukizi ya Ebola, ni lazima nchi wafadhili zitoe fedha na kutengenezwa kwa mfumo maalumu wa afya utakaorahisisha zoezi la kuratibu ikiwa ugonjwa utaripotiwa.

Karibu robo tatu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekimbia makazi yao, huku wengine zaidi ya laki nne wakiishi kama wakimbizi kwenye nchi jirani ikiwemo DRC.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.