Pata taarifa kuu
KENYA-DRC-EBOLA-AFYA

Wizara ya Afya Kenya yatoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Ebola

Wizara ya afya nchini Kenya imesema tahadhari imechukuliwa kuhakikisha kuwa inawakagua abiria wanaoingia katika nchi yake hasa kutoka nchini DRC na eneo la Afrika ya Kati baada ya kuripotiwa kwa maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kusababibisha vifo vya watu 18.

Virusi ya ugonjwa wa Ebola.
Virusi ya ugonjwa wa Ebola. CDC/Frederick A. Murphy
Matangazo ya kibiashara

Tahadhari kama hii imechukuliwa pia na mataifa yote ya Afrika Mashariki ikiwemo Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na hata Nigeria ili kuzuaia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Mapema wiki hii Wizara ya Afya ya Tanzania ilitoa tahadhari kwa wananchi juu ya kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola hasa katika mikoa ambayo inapakana na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuripotiwa wagonjwa wa ugonjwa huo nchini humo.

Shirika la afya duniani WHO linasema limejiandaa na kuchukua tahadhari zote, kuhakikisha kuwa maambukizi hayo yanadhibitiwa.

Wizara ya Afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imethibitisha kuzuka upya kwa ugonjwa wa Ebola na kuua watu 17 katika jimbo la Equateur kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka serikalini, Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Madaktari wasiokuwa na Mipaka ulitarajia kuwasili baadae siku ya Jumatano wiki hii kwenye Kijiji cha Ikoko Impenge kilichoathirika jimboni humo. Dk. Jean Jacques Muyembe, Kiongozi wa maabara ya utafiti wa ugonjwa wa Ebola na magonjwa mengine ya kuambukiza amesema kuna uwezekano mdogo wa ugonjwa huo kusambaa kwenye maeneo mengine

“Hatari ya kusambaa kwa ugonjwa huo ni ndogo kutokana na kwamba vijiji hivyo vilivyoathirika vipo maeneo yasiyofikika kwa urahisi. Ni takriban kilomita 200 msituni na mji wa Mbadaka mji mkuu wa jimbo la Equateur.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya ni kwamba kuna visa 21 vya maambukizi ambapo miongoni mwake watu 18 tayari wamefariki dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.