Pata taarifa kuu
UFARANSA-TABIA NCHI

Mkutano kuhusu tabia nchi kufanyika Paris, Ufaransa

Jumanne hii, Desemba 12, mkutano mpya wa Wakuu wa nchi na Serikali unafanyika katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, ili kuimarisha mkataba juu ya hali ya hewa ulioafikiwa miaka miwili iliyopita. Lengo la kwanza ni kutafuta njia za kufadhili hatua zinazofaa ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika kupambana na ongezeko la joto duniani.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika kupambana na ongezeko la joto duniani. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Kazi itakuwa ngumu zaidi kwani Marekani haitoshiriki mkutano huo baada ya mwezi Juni kutangaza kujitoa katika mktaba huo. Lakini mkutano huu pia ni fursa kwa rais wa Ufaransa kuwa kiongozi katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa hiyo, leo Jumanne, hakutakua na ujumbe rasmi wa Marekani. Lakini washiriki wanajaribu kupuuzia madhara yanayoweza kutokana na kujitoa kwa Marekani, ambayo ni nchi ya pili inayozalisha gesi chafu duniani baada ya China. Miaka miwili iliyopita, ili kuimarisha mkataba kuhusu hali ya hewa ulioafikiwa Paris, rais wa Marekani wa wakati huo Barack Obama na mwenzake wa China Xi Jinping walijikubalisha kudumisha mkataba huo zaidi kuiliko awali katika hali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo, ushiriki wa wadau kutoka Marekani bado ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Na sio tu kwa wasanii kama Di Caprio, au Schwarzenegger, pia gavana wa zamani wa California, lakini pia mabilioneakutoka nchi hiyo, kama vile Bill Gates na Michael Bloomberg, meya wa zamani wa New York.

Wanakuja Paris na viongozi wa miji ya Marekani na majimbo walioelewa dharura ya hali hiyo. Wataweka nguvu zao pamoja na wawekezaji wakubwa ambao wako tayari kutangaza kujitoa, sio katika mkataba kuhusu tabia nchi, lakini sekta zinazochangia katika uzalishaji wa gesi chafu ambazo ni makaa ya mawe na hidrokaboni.

Inabakia matumaini kwamba siku moja, marais wa Marekani watashirikiana na viongozi wanaohusika katika vita hivi dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi. Wakati huo huo, makubaliano yalitengenezwa ili kuokoka kutokuwepo.

Katika video, Emmanuel Macron alimjibu Donald Trump kwa kuwaalika watafiti wote wanasayansi kutoka Marekani wanaotaka kufanya kazi kuhusu hali ya hewa kuja nchini Ufaransa na kuzindua kauli mbiu kwa lugha ya Kiingereza: "Make our planet great again".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.