Pata taarifa kuu
HAITI-HALI YA HEWA

Haiti: kimbunga Matthew kimesababisha vifo vya watu zaidi ya 200

Serikali ya Jimbo la Marekani la Georgia imeamuru Alhamisi hii, Oktoba 6, wakazi wa pwani kuondoka, wakati ambapo kimbuga Matthew kikikaribia. Hatua kama hizo tayari zimechukuliwa na serikali ya jimbo la South Carolina na Florida. Mamlaka ya hali ya hewa imetangaza kuwa kimbunga Matthew kimekua kikijiimarisha katika kiwango cha 4 kinapokaribia Marekani.

Watoto waathirika wa kimbunga Mathew nchini Haiti.
Watoto waathirika wa kimbunga Mathew nchini Haiti. © UNICEF
Matangazo ya kibiashara

Hayo yakijiri idadi ya vifo imeomgezeka nchini Haiti baada kimbunga Matthew kupiga katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Idadi hiyo imetoka kwa watu 108 hadi watu 264 waliopoteza maisha kutokana na kimbunga hiki, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Francois Anick Joseph. Katika wilaya ya Roche--Bateau, kusini mwa nchi, watu wasiopungua 50 walipoteza maisha, Mbunge wa eneo la kusini, Ostin Pierre-Louis, amearifu.

Wengi wa waliopoteza maisha nchini Haiti, walikuwa wakiishi mjini na vijiji vinavyojulikana kwa shughuli za uvuvi katika maeneo ya pwani ya kusini.

Wengi walifariki baada ya kuangukiwa na miti, taka zilizokuwa zikisombwa au hata kusombwa na maji, baada ya mito nyingi kuvunja kingo zao.

Kimbunga Mathew ambacho ndicho kubwa zaidi katika visiwa vya Carebean kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, kimepiga taifa la Bahamas baada ya kupitia Haiti na Cuba.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na serikali ya Haiti na wadau wengine kusambaza vifaa vya usaidizi kwa waathirika wa kimbunga Matthew kilichopiga Haiti hii leo.

UNICEF inasema misaada hiyo ni pamoja na vidonge vya kutakasisha maji na vya kujisafi, wakati huu ambapo watoto zaidi ya Milioni Nne wanatarajiwa kuwa wameathiriwa na zahma hiyo.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti, Marc Vincent amesema kimbunga Matthew ni kibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika miongo ya karibuni na bila shaka madhara yake yatakuwa makubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.