Pata taarifa kuu

HRW inatoa wito kwa Gambia kudumisha marufuku ya tohara kwa wanawake

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) siku ya Ijumaa limewataka wabunge wa Gambia kukataa mswada wa kufuta marufuku ya ukeketaji wa wanawake (FGM), na kuuita "unasumbua sana" kwa haki za wanawake.

Iwapo bunge litapitisha mswada huo mwezi Juni, Gambia itakuwa nchi ya kwanza duniani kubatilisha marufuku ya ukeketaji.
Iwapo bunge litapitisha mswada huo mwezi Juni, Gambia itakuwa nchi ya kwanza duniani kubatilisha marufuku ya ukeketaji. © AP
Matangazo ya kibiashara

Ukeketaji umepigwa marufuku katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi tangu mwaka 2015, lakini wabunge walipiga kura mwezi Machi kwa mswada wenye utata wa kuondoa marufuku hiyo, na kuupeleka kwenye kamati kabla ya mwisho wa kura. Iwapo bunge litapitisha mswada huo mwezi Juni, Gambia itakuwa nchi ya kwanza duniani kubatilisha marufuku ya ukeketaji, HRW imesema katika taarifa iliyopokelewa na shirika la habari la AFP.

"Serikali ya Gambia kutathmini juu ya mswada wa kubatilisha marufuku ya ukeketaji kunatia wasiwasi sana haki za wanawake," amesema Mausi Segun, mkurugenzi wa HRW katika ukanda wa Afrika, aliyenukuliwa katika taarifa hiyo. "Sheria inayopendekezwa itahalalisha ukeketaji nchini na inaweza kuhimiza hatua kama hizo mahali pengine barani Afrika, kudhoofisha maendeleo yaliyopatikana katika kuwalinda wasichana na wanawake kutokana na mila hii mbaya," ameongeza.

Wakati huo huo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF, linasema FGM inarejelea kuondolewa kwa sehemu au jumla ya sehemu ya siri ya nje ya mwanamke au jeraha lingine lolote kwenye sehemu ya siri ya mwanamke kwa sababu zisizo za kimatibabu. Ukeketaji huu ambao ni pamoja na kukatwa unaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya, ikiwa ni pamoja na maambukizi, kuvuja damu, utasa na matatizo wakati wa kujifungua.

Gambia ni mojawapo ya nchi kumi ambako ukeketaji umeenea zaidi: 73% ya wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamefanyiwa utaratibu huu, kulingana na takwimu za UNICEF za mwaka 2024. Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa mwezi Machi inaonyesha kuwa zaidi ya wasichana na wanawake milioni 230 kote ulimwenguni wamelazimika kupitia utaratibu huu.

"Serikali ya Gambia inapaswa kulinda vikali haki za wasichana na wanawake wa Gambia na kukataa mapendekezo yoyote ya kubatilisha au kudhoofisha marufuku ya mwaka 2015 ya ukeketaji," Bw Segun amesema. Mwezi Machi, maafisa wa Umoja wa Mataifa walionya kwamba kupindua marufuku hiyo kuna hatari ya kuweka "mfano hatari" nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.