Pata taarifa kuu

Nigeria: Jeshi lampata msichana wa shule ya Chibok aliyetekwa nyara na Boko Haram

Jeshi la Nigeria limetangaza siku ya Alhamisi kuwa limempata mmoja wa wasichana 276 wa shule ya upili ya Chibok waliotekwa nyara na Boko Haram miaka kumi iliyopita, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Msichana wa shule ya Chibok aliyetekwa nyara Hauwa Joseph ameketi na mtoto wake katika kambi ya Maimalari huko Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, Juni 21, 2022.
Msichana wa shule ya Chibok aliyetekwa nyara Hauwa Joseph ameketi na mtoto wake katika kambi ya Maimalari huko Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, Juni 21, 2022. © Audu MARTE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Lydia "aliokolewa akiwa pamoja na watoto wake watatu" karibu na mji wa Ngoshe katika jimbo la Borno, jeshi limetangaza katika taarifa siku ya Alhamisi. Kwa mujibu wa jeshi hilo, msichana huyo ana ujauzito wa miezi mitano. Utekaji nyara mkubwa katika mji wa Chibok ulizua kilio kikubwa duniani kote mwaka wa 2014, na kuibua kampeni ya kimataifa iliyoitwa "Bring back our girls". Takriban 100 kati yao hawajulikani waliko.

Kwa miaka mingi, jeshi limeokoa wasichana kadhaa wa shulehilo upili, ambao wengi wao walilazimishwa kuolewa na watekaji nyara wao wa kijihadi. Wanachama wa Boko Haram leo wamedhoofishwa na operesheni za jeshi, ambalo limechukua maeneo makubwa yaliyokuwa yakishikiliwa na kundi hili la kijihadi, na mapambano ya ndani na kundi linalopingana na kundi la Islamic State Afrika Magharibi (Iswap), hata hivyo, linaendelea kufanya mashambulizi kaskazini mwa Nigeria.

Boko Haram hasa hushambulia maeneo ya mbali, na kulenga misafara inayoondoka katika miji iliyolindwa na jeshi. Uasi wa wanajihadi kaskazini mwa Nigeria umesababisha vifo vya watu zaidi ya 40,000 na milioni mbili kuyahama makazi yao tangu mwaka 2009.

Utekaji nyara mkubwa unasalia kuwa wasiwasi mkubwa nchini Nigeria, huku kukiwa na ongezeko la makundi ya wahalifu wenye silaha wanaoitwa "majambazi" wanaoendesha shughuli zao kwenye barabara kuu, katika nyumba za waathiriwa na hata shuleni ili kupata fidia. Zaidi ya wanafunzi 1,680 walitekwa nyara kutoka shule za Nigeria kati ya mwaka 2014 na 2022, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Save the Children.

Mwezi Machi, zaidi ya watoto 130 walitekwa nyara kutoka shuleni mwao na watu wenye silaha katika jimbo la kaskazini-magharibi la Kaduna. Utekaji nyara huu ni mojawapo ya matukio muhimu zaidi ya utekaji nyara katika miaka ya hivi majuzi nchini Nigeria. Jeshi la Nigeria limesema wanafunzi wote hao waliokolewa wiki kadhaa baadaye katika jimbo jirani la Zamfara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.