Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Watu 10 wafariki katika mlipuko wa bomu kaskazini mashariki mwa Nigeria

Takriban watu 10 wamefariki na wengine 23 kujeruhiwa na mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini kaskazini mashariki mwa Nigeria, eneo ambalo limekumbwa na mashambulizi ya wanajihadi kwa miaka kadhaa. Waathiriwa walikuwa wakulima na wavuvi ambao waliondoka katika mji wa Monguno kwenda kwenye ufuo wa Ziwa Chad.

Katika miaka ya hivi karibuni, ghasia za wanajihadi kutoka Nigeria zimeenea hadi nchi jirani za Niger, Chad na Cameroon.
Katika miaka ya hivi karibuni, ghasia za wanajihadi kutoka Nigeria zimeenea hadi nchi jirani za Niger, Chad na Cameroon. AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Gari lao lilikanyaga bomu la ardhini linaloaminika kutegwa na wanajihadi wa Islamic State Afrika Magharibi (ISWAP) wanaohusishwa na ISIS, duru zimesema. Wanachama wa ISWAP wamerudishwa nyuma kutoka maeneo kadhaa waliyodhibiti, lakini bado wako katika maeneo ya mbali ambapo wanashambulia misafara ya magari yanayotoka miji inayolindwa na jeshi.

"Gari lilikanyaga kilipuzi kilichowekwa kwenye barabara karibu na kambi ya Mbu, kilomita tatu kutoka Monguno mwendo wa 3:30 asubuhi, na kusababisha mlipuko ambao uliharibu gari," amesema Musa Kaka, mwanachama wa wanamgambo wanaopinga wanajihadi ambao husaidia jeshi la Nigeria. "Tumepata miili 10 na majeruhi 23 katika eneo la tukio," ameongeza Bw. Kaka.

Waliofariki walizikwa siku ya Jumatano, huku waliojeruhiwa wakipelekwa katika hospitali ya jiji, amesema Bello Adamu, mwanamgambo mwingine anayepinga jihadi. Kiongozi mwingine wa wanamgambo, Umar Ari, pia amethibitisha idadi ya waliouawa. Shirika la habari la AFP linasema limejitahidi kuongea na jeshi la Nigeria ili kuweza kutoa maoni yake kuhusu tukio hili, bila majibu hadi sasa.

ISWAP, ambayo ilijitenga mwaka 2016 kutoka kwa kundi hasimu la Boko Haram, sasa inatawala katika eneo la Ziwa Chad. Makundi hayo mawili ya wanajihadi yanajulikana kwa kutega mabomu ya ardhini kwenye barabara na barabara kuu ili kulenga misafara ya magari ya jeshi na raia kama sehemu ya uasi wao ambao umedumu tangu mwaka 2009 na kusababisha vifo vya watu 40,000 na zaidi ya milioni mbili kuyahama makazi yao. Katika miaka ya hivi karibuni, ghasia za wanajihadi zimeenea katika nchi jirani za Niger, Chad na Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.