Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-MAANDAMANO

Togo: Upinzani unadumisha maandamano yake licha ya marufuku ya mamlaka

Vyama kadhaa vya upinzani nchiniTogo vimetoa wito kwa raia siku ya Alhamisi kushiriki "kwa wingi" katika maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijumaa na Jumamosi huko Lomé kupinga Katiba Mpya licha ya marufuku ya mamlaka.

Mwezi Machi mwaka jana, waandishi wawili wa habari wa Togo walihukumiwa bila kuwepo mahakamani kifungo cha miaka mitatu jela kwa "kudharau mamlaka" na "kueneza uongo kwenye mitandao ya kijamii".
Mwezi Machi mwaka jana, waandishi wawili wa habari wa Togo walihukumiwa bila kuwepo mahakamani kifungo cha miaka mitatu jela kwa "kudharau mamlaka" na "kueneza uongo kwenye mitandao ya kijamii". © Reuters / Noel Kokou Tadegnon
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa upinzani na mashirika ya kiraia walitoa wito kwa Watogo katika mkutano na waandishi wa habari "kuhudhuria kwa wingi maandamano ya Aprili 12 na 13 ya kukataa Katiba iliyochafuliwa ambayo serikali na washirika wake wanataka kuwalazimisha.

Waziri wa Mmabo ya Ndani Hodabalo Awaté alipiga marufuku maandamano haya kwa kutofuata tarehe ya mwisho ya tamko na uchaguzi wa njia ambayo "inakiuka" rasimu hiyo. Kwa upande wake, serikali ilithibitisha katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumanne jioni kwamba waandaaji wanapanga kupanua maandamano "katika miji yote kwa kuwaondoa shuleni wanafunzi na kushambulia kwa utaratibu nyumba za wabunge walengwa hapo awali."

"Uongo na kejeli," alijibu Paul Dodji Apévon, mkuu wa chama cha Democratic Forces for the Republic (FDR). "Huu ni ujanja wa kututisha na kuzuia maandamano hayo, tumewajulisha watu kisheria, hakuna sababu ya sisi kuambiwa kuwa hatuwezi kuandamana kesho na Jumamosi 1Aprili 13," amesema.

"Lazima tupambane, kwa sababu tunakabiliwa na mapinduzi yaliyofanywa na mtu ambaye lengo lake pekee ni kubakia madarakani milele," amesema Jean Pierre Fabre, mkuu wa hama cha Muungano wa Kitaifa wa Mabadiliko (ANC).

Huko Togo, maandamano ya barabarani yamepigwa marufuku tangu 2022, baada ya shambulio kwenye soko kubwa huko Lomé wakati askari mmoja aliuawa. Togo imepanga uchaguzi wa wabunge utakaofanyika Aprili 29, baada ya kuahirishwa katika muktadha wa kupitishwa kwa Katiba mpya mwishoni mwa mwezi wa Machi.

Uchaguzi hui ulikuwa ufanyike tarehe 20 Aprili, lakini serikali ya Togo iliahirisha ili kufanya mashauriano kuhusu Katiba mpya, ambayo inachukuliwa na vyama kadhaa vya upinzani kama mbinu ya kumweka Rais Faure Gnassingbé madarakani kwa muda mrefu zaidi.

Viongozi wa upinzani hawana nia ya kususia uchaguzi huu, kama walivyofanya mwaka wa 2018 kushutumu "makosa" katika sensa ya uchaguzi. Rais Gnassingbé amekuwa madarakani tangu 2005. Alimrithi baba yake ambaye alitumia karibu miaka 38 akiwa mkuu wa Togo baada ya mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.