Pata taarifa kuu

Ethiopia: Mpinzani wa Oromo aliyeachiliwa hivi majuzi auawa kwa kupigwa risasi

Kiongozi wa upinzani nchini Ethiopia, Bate Urgessa, amepatikana akiwa amekufa siku ya Jumatano asubuhi, baada ya kupigwa risasi hadi kufa, saa chache baada ya kukamatwa na vikosi vya serikali katikati mwa Ethiopia, chama chake, Oromo Liberation Front (OLF), kimetangaza.

Mnamo Februari 22, Bate Urgessa alikamatwa huko Addis Ababa akiwa na Antoine Galindo, mwandishi wa habari wa chapisho maalum la Africa Intelligence, ambaye alikuwa akizungumza naye. Wanaume hao wawili walishutumiwa kwa "kula njama" na makundi yenye silaha "kuanzisha machafuko" nchini Ethiopia. Aliachiliwa kwa dhamana mnamo Machi 6, wiki moja baada ya Bw. Galindo.
Mnamo Februari 22, Bate Urgessa alikamatwa huko Addis Ababa akiwa na Antoine Galindo, mwandishi wa habari wa chapisho maalum la Africa Intelligence, ambaye alikuwa akizungumza naye. Wanaume hao wawili walishutumiwa kwa "kula njama" na makundi yenye silaha "kuanzisha machafuko" nchini Ethiopia. Aliachiliwa kwa dhamana mnamo Machi 6, wiki moja baada ya Bw. Galindo. © DR
Matangazo ya kibiashara

Bate Urgessa, 41, aliachiliwa kwa dhamana mwezi mmoja uliopita, baada ya siku 15 za kuzuiliwa kufuatia kukamatwa kwake mjini Addis Ababa akiwa na mwandishi wa habari wa Ufaransa, Antoine Galindo.

siku ya Jumanne karibu 11:00 jioni  saa za ndani, Bate alikamatwa na vikosi vya serikali katika hoteli ya Meki" na kisha kupelekwa moja kwa moja katika kituo cha kizuizini cha eneo hilo, linachopatikana kilomita 150 kusini mwa Addis Ababa, katika jimbo la kikanda la Oromia ambalo linazunguka mji mkuu wa Ethiopia, Lemi Gemechu, msemaji wa OLF, chama cha upinzani kilichosajiliwa kisheria, ameliambia shirika la habari la AFP. "Familia yake imethibitisha kuwa aligunduliwa akiwa amekufa kwenye barabara (...) katika viunga vya Meki" Jumatano asubuhi mwendo wa saa 3:00 asubuhi, saa za ndan na washirikawake wa karibu wamebaini kuwa "amepigwa risasi na kuuawa" , ameongeza, bila kuweka mbele dhana yoyote kuhusu mhusika wa mauaji hayo.

Pia alisema hajui iwapo watu waliomkamata Bw. Bate ni wa vikosi vya shirikisho au vya kikanda. Serikali ya shirikisho haijajibu kwa sasa, lakini mamlaka za kikanda zimekataa kuhusika katika "mauaji".

"Serikali ya jimbo la Oromia linalaani vikali mauaji ya Bate Urgessa, ambayo yalifanywa na kundi lisilojulikana," unasema ujumbe kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook. Meki ni mji alikozaliwa Bate Urgessa, ambaye alikuwa kiongozi wa OLF, chama ambachokiinalenga kuwa sauti kwa ajili ya Waoromo, wengi zaidi kati ya takriban watu makaila 80 nchini Ethiopia.

"Mauaji ya kikatili"

Katika taarifa, chama chake kilishutumu "mauaji ya kikatili" na kukumbusha kuwa, mnamo 2020, mwimbaji maarufu wa Oromo Hachalu Hundessa, mshika bendera wa jamii, ambaye mauaji yake yalisababisha ghasia za siku kadhaa na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200. "Mauaji yasiyo ya haki" ya "vigogo wa kisiasa wa kitamaduni wa Oromo" yanalenga "kuwanyamazisha Waoromo kwa miaka na miongo," chama cha OLF kmesema, kikibaini kwamba kilikuwa kikifanya uchunguzi wake chenyewe kuhusu kifo cha kiongozi wake.

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia (EHRC) "inataka uchunguzi wa haraka, usio na upendeleo na wa kina" kuhusu kifo cha Bw. Bate, "ili waliohusika wawajibishwe", amesema kwenye mtandao wa X Daniel Bekele, mkuu wa taasisi hii ya umma lakini kisheria hujitegemea.

Mnamo mwaka 2022, EHRC ilihusisha vikosi vya usalama katika "mauaji yasiyo ya haki" ya raia 14 huko Oromia, wanachama wa mfumo wa Gada wa utawala wa jadi wa Oromo. Mkurugenzi wa Afrika Mashariki wa shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch (HRW), Laetitia Bader alitoa wito wa "uchunguzi wa kuaminika", akikumbusha kuwa Bw. Bate "amekuwa akizuiliwa mara kwa mara kinyume cha sheria".

Bw. Bate alikuwa na uzoefu wa jela za Ethiopia mara kadhaa, iwe chini ya serikali ya muungano ya zamani ya EPRDF (1991-2018) au chini ya ile ya Waziri Mkuu wa sasa Abiy Ahmed aliyemrithi. Mnamo mwaka 2022, aliachiliwa kwa sababu za kiafya baada ya mwaka mmoja akiwa kizuizini.

Viongozi hufungwa

Mnamo Februari 22, Bate Urgessa alikamatwa huko Addis Ababa akiwa na Antoine Galindo, mwandishi wa habari wa chapisho maalum la Africa Intelligence, ambaye alikuwa akizungumza naye. Wanaume hao wawili walishutumiwa kwa "kula njama" na makundi yenye silaha "kuanzisha machafuko" nchini Ethiopia. Aliachiliwa kwa dhamana mnamo Machi 6, wiki moja baada ya Bw. Galindo.

Kinyume cha sheria na kuwa na tawi la kijeshi hadi mwaka 2018, OLF iliachana na mapambano ya silaha baada ya kupewa msamaha, kutambuliwa kisheria na kurudi kutoka uhamishoni kwa viongozi wake, wakati Bw. Abiy alipoingia madarakani - yeye mwenyewe Oromo na baba yake - ambayo iliambatana na ufunguzi wa nafasi ya kisiasa. Lakini OLF tangu wakati huo imeishutumu serikali ya Bw. Abiy kwa kufunga ofisi zake nyingi, kuzuia ushiriki wake katika uchaguzi na kuwafunga maafisa wake kadhaa, ambao baadhi yao wamezuiliwa kwa miaka kadhaa bila kesi.

Baada ya kukataa kutoa kuweka chini silaha mnamo mwaka 2018, sehemu ya OLF iligawanyika na kuunda Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA). Ikiwa imeainishwa kama "kundi la kigaidi" nchini Ethiopia, OLA hupigana kutoka kwa vikosi vya shirikisho au vikosi vinavyoshirikiana na serikali ya mkoa huko Oromia, eneo kubwa na lenye watu wengi zaidi la Ethiopia, lenye takriban milioni 40 wakaazi wa Oromo.

Mzozo wa Oromia unaambatana na mauaji ya jamii na hakuna upande unaoonekana kuwa na manufaa yoyote ya kijeshi. Duru mbili za mazungumzo zilibaki bila mafanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.