Pata taarifa kuu

Sissi aanza muhula wake wa tatu katikati ya mzozo mkubwa wa kiuchumi

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi ataapishwa wiki hii kuanza muhula wake wa tatu mfululizo, katikati ya hali mbaya ya kiuchumi inayoambatana na "janga" la haki za binadamu, wataalam wanasema.

Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi akihutubia bunge baada ya kuapishwa kwa muhula wa pili wa miaka minne, mjini Cairo, Juni 2, 2018.
Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi akihutubia bunge baada ya kuapishwa kwa muhula wa pili wa miaka minne, mjini Cairo, Juni 2, 2018. © AP
Matangazo ya kibiashara

Akiwa madarakani kwa muongo mmoja, Bw. Sissi, 69, ataanza muhula huu mwingine siku ya Jumatano, zaidi ya miezi mitatu baada ya kuchaguliwa tena kwa 89.6% ya kura dhidi ya wagombea watatu ambao hawakujulikana sana na umma. Muhula wake mwingine, wa miaka sita, unatakiwa kuwa wa mwisho kwa mujibu wa Katiba ya Misri.

Bw. Sissi atakula kiapo siku ya Jumanne asubuhi mbele ya Bunge katika mji mkuu mpya wa utawala, takriban kilomita hamsini mashariki mwa Cairo, kulingana na mbunge Moustafa Bakri, anayejulikana kuwa karibu na mamlaka. Kulingana mbunge huyo, serikali inapaswa kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu baada ya kuapishwa kwa Bw. Sissi, ingawa "Katiba hailazimishi kufanya hivyo."

Bw. Sisisi anaanza muhula wake mwingine akiwa na theluthi mbili ya wakazi milioni 106 wanaoishi chini au juu ya mstari wa umaskini. Misri pia imejikuta thamani ya sarafu yake ikigawanywa na tatu na deni lake kuongezeka kwa kiasi hicho. Na kutokana na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni unaodumaza biashara, gharama ya maisha katika uchumi unaotegemea uagizaji bidhaa imeendelea kupanda, huku mfumuko wa bei ukipanda kwa 35%.

Mabilioni ya dola

Katika robo ya kwanza ya mwaka 2024, Cairo ilinufaika na utitiri wa makumi ya mabilioni ya dola, ikiwa ni pamoja na bilioni 35 kutoka Falme za Kiarabu na kuongezwa kwa bilioni 5 kutoka kwa mkopo wa awali wa bilioni 3 kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa. Fedha hizi hata hivyo zinaambatana na masharti magumu yanayowekwa na wafadhili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.