Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Rais Erdogan wa Uturuki kuzuru Misri Jumatano

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi atampokea mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mjini Cairo siku ya Jumatano, ziara ambayo haijawahi kushuhudiwa inayonuiwa kubiresha maridhiano baada ya zaidi ya muongo mmoja wa mafarakano kati ya nchi hizo mbili.

Siku ya Jumatatu, Bw. Erdogan alisema anaenda Falme za Kiarabu na kisha Misri ili "kuona nini zaidi kinaweza kufanywa kwa ajili ya ndugu zetu huko Gaza."
Siku ya Jumatatu, Bw. Erdogan alisema anaenda Falme za Kiarabu na kisha Misri ili "kuona nini zaidi kinaweza kufanywa kwa ajili ya ndugu zetu huko Gaza." AP - Denes Erdos
Matangazo ya kibiashara

 

Siku ya Jumatatu, Bw. Erdogan alisema anaenda Falme za Kiarabu na kisha Misri ili "kuona nini zaidi kinaweza kufanywa kwa ajili ya ndugu zetu huko Gaza." Aliongeza kuwa Ankara ilikuwa inafanya "kila kitu kukomesha umwagaji damu" huku zaidi ya Wapalestina 28,000 wakiuawa, idadi kubwa ya raia, kwa mujibu wa serikali ya Hamas, katika mashambulizi yaliyoanzishwa na Israel kulipiza kisasi shambulio la wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina kusini mwa Israeli mnamo Oktoba 7.

Shambulio hili ambalo halijawahi kushuhudiwa lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,160 upande wa Israel, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP ikijikita kwenye data rasmi za Israeli. Rais wa Uturuki alizuru Misri mara ya mwisho mwaka 2012 alipokuwa waziri mkuu. Mohamed Morsi, mshirika mkubwa wa Ankara, wakati huo alikuwa rais wa nchi hiyo.

Waziri wake wa Ulinzi, Abdel Fattah al-Sissi, alimpindua mwaka wa 2013 na tangu wakati huo, Bw. Erdogan alikuwa akirejelea kauli yake kwamba "hatawahi" kuzungumza na "mtu kama yeye". Hata hivyo uhusiano kati ya wawili hao umeongezeka, maslahi yao sasa yanaungana katika mizozo kadhaa ya kikanda ikiwa ni pamoja na Sudan na Ukanda wa Gaza.

Walipeana mkono kwa mara yao ya kwanza kabisa mnamo mezi wa Novemba 2022 wakati wa Kombe la Dunia la FIFA nchini Qatar, nchi nyingine ambayo Misri iliungana nayo hivi karibuni baada ya kuishutumu kwa ukaribu na kundi la Muslim Brotherhood. Pia walizungumza siku moja baada ya tetemeko la ardhi la Februari 6, 2023 ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 50,000 nchini Uturuki. Na mwezi Julai, mabalozi waliteuliwa kutoka pande zote mbili. Mnamo mwezi wa Septemba, watu hao wawili walizungumza kwa mara ya kwanza ana kwa ana kando ya mkutano wa kilele wa G20 huko New Delhi.

Ikiwa kisiasa walitofautiana kwa kipindi kirefu, Misri na Uturuki zinaunga mkono serikali mbili zinazopingana nchini Libya, uhusiano wa kibiashara umesalia kuwa mzuri: Ankara ni mshirika wa tano wa kibiashara wa Cairo. Mapema mwezi Februari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alitangaza kuiuzia Misri ndege zisizo na rubani.

Kuhusu suala la Gaza, Bw. Erdogan, ambaye aliielezea Israel kama "taifa la kigaidi" na Hamas kama "kundi la wakombozi", alimuitisha nyumbani balozi wa Uturuki mjini Tel Aviv mwanzoni mwa mwezi Novemba, huku akiona kuwa haiwezekani "kuvunja kabisa" uhuano na Israeli.

Kabla ya Oktoba 7, viongozi kadhaa wa kisiasa wa Hamas waliishi Istanbul. Tangu wakati huo wameombwa kimya kimya kuondoka. Tangu kuanza kwa mzozo huko Gaza, Bw. Erdogan alipendekeza kufanya upatanishi lakini majadiliano juu ya usitishwaji mapigano hadi sasa yanaongozwa na Qatar na Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.