Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-RUSHWA

Uchaguzi wa maseneta na magavana: Rais Tshisekedi awaonya watoaji na wapokeaji rushwa

Rais Félix-Antoine Tshisekedi anaonya, ndani ya mfumo wa uchaguzi wa maseneta na magavana, watoaji na wapokeaji rushwa, Waziri wa Sheria, Rose Mutombo ametangaza hivi punde Jumanne usiku Machi 12.

Uchaguzi wa maseneta pamoja na ule wa magavana na manaibu magavana wa mikoa ambao awali uliopangwa kufanyika Machi 31 na Aprili 7, 2024 mtawalia, uliahirishwa kwa wiki tatu. Kalenda iliyorekebishwa, kama ilivyochapishwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI), inatoa fursa kwa uchaguzi wa maseneta mnamo Aprili 21 na kura ya magavana na manaibu magavana Aprili 28.
Uchaguzi wa maseneta pamoja na ule wa magavana na manaibu magavana wa mikoa ambao awali uliopangwa kufanyika Machi 31 na Aprili 7, 2024 mtawalia, uliahirishwa kwa wiki tatu. Kalenda iliyorekebishwa, kama ilivyochapishwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI), inatoa fursa kwa uchaguzi wa maseneta mnamo Aprili 21 na kura ya magavana na manaibu magavana Aprili 28. AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa baada ya mazungumzo yake, siku ya Jumanne katika Jiji la Umoja wa Afrika, na Rais Félix-Antoine Tshisekedi, kuhusu tabia ya wabunge mbalimbali wa mikoa ambao wanauza kura zao kwa wagombea wa nafasi za maseneta na magavana, inaripoti taarifa kutoka Kitengo cha Mawasiliano ya ofisi ya rais.

"Katika nafasi yake ya mdhamini wa utendaji kazi mzuri wa taasisi, Mkuu wa Nchi alimtaka Bi. Mutombo ajadiliane na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mahakama Kuu" ili aweze kuvuta hisia za Wanasheria Wakuu mbalimbali kuhusu tetesi hizi zote za rushwa, inasema taarifa hiyo.

“Tabia hii inabidi ikomeshwe. Hatuwezi kuendelea kukubali ufisadi wa wazi namna hii. Lazima kuwe na vikwazo vikali kwa yeyote atakayepatikana akiuza kura yake. Yeyote atakayekamatwa atakabiliwa na hatua kali kulingana na sheria,” amesema Waziri wa Sheria wa DRC Rose Mutombo, kwa mujibu wa Radio OKAPI.

Uchaguzi wa maseneta pamoja na ule wa magavana na manaibu magavana wa mikoa ambao awali uliopangwa kufanyika Machi 31 na Aprili 7, 2024 mtawalia, uliahirishwa kwa wiki tatu. Kalenda iliyorekebishwa, kama ilivyochapishwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI), inatoa fursa kwa uchaguzi wa maseneta mnamo Aprili 21 na kura ya magavana na manaibu magavana Aprili 28.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.