Pata taarifa kuu

Guinea: Wanajeshi kurejesha utawala wa kiraia mwaka wa 2025

Nairobi – Waziri Mkuu mpya wa Guinea, Amadou Oury Bah, amedokeza kuwa wanajeshi walionyakua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2021 watachelewesha kurejea kwa utawala wa kiraia hadi angalau mwaka 2025.

Waziri Mkuu mpya wa Guinea, Amadou Oury Bah.
Waziri Mkuu mpya wa Guinea, Amadou Oury Bah. © Facebook/Bah Oury
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano yake na idhaa yetu ya Kifaransa, waziri mkuu Bah, amesema wanahitaji kwanza kutatua mdororo wa kiuchumi unaoikabili nchi hiyo pamoja na kupata maridhiano ya kitaifa.

Kuhusu Kura ya maoni ya mabadiliko ya katiba, waziri mkuu huyo amesema inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Kauli yake, anaitoa licha ya mwezi uliopita, Serikali ya mpito ya kijeshi kushuhudia maandamano makubwa ya kwanza ya raia kupinga kupanda kwa gharama ya maisha nchini humo.

Kauli ya waziri mkuu Bah, inafuta kauli iliyotolewa na Jenerali Mamady Doumbouya, ambaye wakati akiingia madarakani mwezi Septemba 2021, aliahidi kurejesha utawala wa kiraia ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.