Pata taarifa kuu

Sudan: Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kusitishwa kwa mapigano wakati wa Ramadhani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito Alhamisi hii, Machi 7, kwa wapiganaji nchini Sudan kwa ajili ya kusitisha mapigano wakati wa mwezi wa Ramadhani, kuheshimu "maadili" ya mwezi mtukufu kwa Waislamu wakati mzozo wa kibinadamu unafikia viwango vya mgogoro mkubwa. 

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo almaarufu Hemedti (kulia).
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (kushoto) na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo almaarufu Hemedti (kulia). © AP
Matangazo ya kibiashara

“Baada ya siku chache, mwezi mtukufu wa Ramadhani utaanza. Kwa hivyo kutoka mahali hapa leo, ninatoa wito. Natoa wito kwa pande zote nchini Sudan kuheshimu maadili ya mwezi wa Ramadhani kwa kukomesha uhasama katika mwezi huo,” ameuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja w Mataifa.

Huku mfungo wa mwez wa Ramadhani ukielekea kuanza Jumapili, kulingana na kuonekana kwa mwezi mpya, baraza la usalma la Umoja wa Mataifa linataka kupiga kura haraka, labda siku ya Ijumaa.

Sudan ilitumbukia kwenye machafuko mwezi Aprili mwaka jana, wakati mvutano wa muda mrefu kati ya jeshi lake linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Burhan na vikosi vya wanamgambo, (RSF) vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo vilipoingia katika mapigano ya mitaani katika mji mkuu, Khartoum.

Mapigano hayo yameenea katika maeneo mengine ya nchi, hususan maeneo ya mijini, lakini katika eneo la Darfur, magharibi mwa Sudan, yamechukua sura tofauti, kwa mashambulizi ya kikatili ya vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), ambao wengi wao ni Waarabu, dhidi ya raia wenye asili ya Afrika. Maelfu ya watu waliuawa.

Miaka 20 iliyopita, Darfur ilifanana na mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita, hasa uliofanywa na wanamgambo wa Kiarabu wa Janjaweed dhidi ya watu wanaojitambulisha kama Afrika ya Kati au Mashariki.

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Karim Khan alisema mwishoni mwa mwezi wa Januari kwamba kuna sababu ya kuamini kwamba pande zote mbili katika mzozo wa sasa zinafanya uhalifu wa kivita unaowezekana, uhalifu dhidi ya ubinadamu au mauaji ya halaiki huko Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.