Pata taarifa kuu

Sudan: Ripoti ya Umoja wa Mataifa inashutumu RSF kutekeleza mauaji El-Geneina

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, kusonga mbele kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Jenerali Hemedti huko Darfur mwaka jana kuliambatana na mauaji ya kikabila, hasa katika mji mkuu wa Darfur Magharibi, El-Geneina, ambapo ghasia zinaweza, kulingana na wataalam hawa, kufikia uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Wakaazi wakitembea kati ya vifusi katika mji mkuu wa Darfur Magharibi wa El-Geneina, baada ya shambulio la Aprili 29, 2023.
Wakaazi wakitembea kati ya vifusi katika mji mkuu wa Darfur Magharibi wa El-Geneina, baada ya shambulio la Aprili 29, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Katika mji wa El-Geneina pekee, kati ya watu 10,000 na 15,000 - raia - waliuawa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaripoti. Kutekwa kwa jiji hili kulifanyika kwa hatua mbili, wanaeleza. Shambulio la mwezi Juni, na kusababisha kuhama kwa watu kutoka jamii ya Massalit katika kambi za wakimbizi wa ndani. Na shambulio la mwisho mnamo mwezi wa Novemba mwaka jana.

Baada ya kulifukuza jeshi, wanamgambo hao wa RSF - chini ya uongozi wa kaka wa Jenerali Hemedti - kisha waliwashambulia raia majumbani mwao, katika kambi za wakimbizi na barabarani walipokuwa wakikimbilia kuelekea Chad. Vijana kutoka kabila la Massalit walilengwa, wameongeza wataalam hawa, ambao wanaripoti mauaji ya kikatili, ubakaji wa wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 14, uharibifu wa mali, na uporaji wa mali.

Watu kutoka jamii ya Massalit waliutoroka mji wa El-Geneina na viunga vyake na kusalia tupu. "Mashambulizi hayo yalipangwa, kuratibiwa na kutekelezwa na RSF na wanamgambo washirika wao wa Kiarabu," ripoti ya Umoja wa Mataifa ilnasema, ambayo inahitimisha kuwa ukiukwaji huu unaweza kujumuisha uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.