Pata taarifa kuu

Mali: Kanali Alpha Yaya Sangaré akamatwa Bamako

Kanali Alpha Yaya Sangaré, mwandishi wa kitabu kinachohusisha Vikosi vya Ulinzi na Usalama (FDS) kwa mauaji na unyanyasaji, alikamatwa siku ya Jumamosi jioni katika mji mkuu wa Mali, Bamako. 

Vikosi vya usalama na ulinzi vya Mali (FDS) vinahuishwa katika mauaji ya raia.
Vikosi vya usalama na ulinzi vya Mali (FDS) vinahuishwa katika mauaji ya raia. © AFP PHOTO / Souleymane AG ANARA
Matangazo ya kibiashara

Katika kitabu chake "Mali: Changamoto ya Ugaidi katika Afrika", mwandishi anasimulia, kwa mfano, kwamba FDS ilijihusisha na mauaji na visa mbalimbali vya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya raia waliokamatwa na wanaoshukiwa kuwa wanajihadi. 

Pia ananukuu ripoti kutoka kwa vyama vya kigeni vya haki za binadamu vinavyoshutumu mtazamo wa jeshi kwa raia waliokamatwa wakati wa operesheni za "kupambana na ugaidi".

Katika kitabu hiki chenye kurasa 400, Kanali Apha Yaya Sangaré anazungumzia hasa suala la haki za binadamu ndani ya jeshi la Mali. "Tangu mwaka 2016," anaandika, "FDS imetekeleza mauaji dhidi ya watu wanaoshutumiwa kuwa sehemu ya makundi ya kigaidi."

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Ulinzi imelaani maoni haya, ikakumbusha kwamba kitabu hicho kilitolewa bila idhni kutoka kwa jeshi na ikatangaza vikwazo dhidi ya afisa huyo.

Maelezo mengine yanaibua sintofahamu. Katika chumba ambacho sherehe ya uzinduzi wa kitabu ilifanyika, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Utawala wa Wilaya na msemaji wa serikali, Kanali Abdoulaye Maïga, alikuwepo. Yeye ni mwanafunzi mwenza wa mwandishi wa kitabu hicho, wote wanatoka katika kundi la 23 la chuo cha maafisa cha Koulikoro, kiliyoko kilomita 50 kutoka Bamako.

kutokana na sintofahamu hiyo, katika taarifa iliyochapishwa siku ya Jumamosi, waziri na msemaji kwa upande wake wanatofautiana na kazi hiyo. Anadai kuwa alisoma tu kitabu hicho katika chumba ambacho sherehe ya kutangaza kitabu hicho ilifanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.