Pata taarifa kuu
USALAMA-AMANI

Mali: Utata baada ya kuchapishwa kwa kitabu cha kanali kinachoibua 'mauaji' ya jeshi

Kitabu kimezua utata huko Bamako. Nchini Mali: Changamoto ya Ugaidi barani Afrika, afisa mmoja wa cheo cha kanali katika jeshi la Mali anajadili ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la Mali, FAMA. Wizara ya Ulinzi ya Mali imekanusha vifungu hivi katika kitabu hicho ambacho kinalitia hatiani jeshi la nchi hiyo.

Askari wa Mali FAMA (picha ya kielelezo).
Askari wa Mali FAMA (picha ya kielelezo). PHILIPPE DESMAZES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Katika kitabu hiki chenye kurasa 400, Kanali Apha Yaya Sangaré anazungumzia hasa suala la haki za binadamu ndani ya jeshi la Mali. "Tangu mwaka 2016," anaandika, "FDS imetekeleza mauaji dhidi ya watu wanaoshutumiwa kuwa sehemu ya makundi ya kigaidi."

Pia ananukuu ripoti kutoka kwa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu ambayo yanashutumu ukiukwaji unaohusishwa na FDS, juu ya misheni ya kupambana na ugaidi.

Wizara ya Ulinzi ya Mali haikuthamini hata kidogo. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, imelaani maoni haya, ikakumbusha kwamba kitabu hicho kilitolewa bila idhni kutoka kwa jeshi na ikatangaza vikwazo dhidi ya afisa huyo.

Maelezo mengine yanaibua sintofahamu. Katika chumba ambacho sherehe ya uzinduzi wa kitabu ilifanyika, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Utawala wa Wilaya na msemaji wa serikali, Kanali Abdoulaye Maïga, alikuwepo. Yeye ni mwanafunzi mwenza wa mwandishi wa kitabu hicho, wote wanatoka katika kundi la 23 la chuo cha maafisa cha Koulikoro, kiliyoko kilomita 50 kutoka Bamako.

kutokana na sintofahamu hiyo, katika taarifa iliyochapishwa siku ya Jumamosi, waziri na msemaji kwa upande wake wanatofautiana na kazi hiyo. Anadai kuwa alisoma tu kitabu hicho katika chumba ambacho sherehe ya kutangaza kitabu hicho ilifanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.